Ksii Ksii, Halloo dada eeh!Nisubiri basi !
>> Wednesday, February 14, 2007
Inasemekana wanawake hutokea sayari ya zuhura(Venus) na wanaume hutokea mars(sijui kiswahili chake). Basi kutokana na kutokea katika sayari mbili tofauti basi kasheshe haziishi.
Chakutisha hata urafiki kati ya mwanamke na mwanaume unachokochoko zake.
Inasemekana kuna watu wengi duniani hupenda kuhalalisha kuwa urafiki kati ya mwanaume na mwanamke hauwezekani bila ngono kuhusishwa. Wengine wanasema mwanamke ananguvu ya kutomtamani mwanamme. Hivyo mwanamke asiyevutia wanaume ndio pekee akaribishwaye kama rafiki wa kawaida na mwanaume. Huwa najiuliza, hivi kuna mwanamke asiyevutia mwanaume lakini?Si tushaambiwa kuwa kizuri kijichoni mwa mtazamaji lakini?
Halafu kunaimani kuwa ni wanaume tu huwa wanafukuzia wanawake. Nisikufiche baada ya kutembea hapa duniani mara nyingi tu nimekuta mwanaume kabanwa kwenye kona na mwanamke anapewa kauli halafu yeye ndio anajikanyaga. Kwa bahati nzuri mimi kwa mara yakwanza ilinitokea nikiwa darasa la sita, nilipopigwa kauli na mwanadada mpaka nikawa naona noma kwa sababu watu walishuhudia halafu wakaanza kunitania kwa jinsi nilivyoishiwa kauli.
Swali:
Hivi hizi choko choko za mahusiano kati ya mwanamke na mwanaume, hutokana na tamaduni za jamii au hata baolojia ya binadamu hucheza kipengele?
Haya siku hii ya leo watu wengi husherekea VALENTINE' Day. Husherehekewa sehemu nyingi na wapendanao, nikiwa na maana wapenzi, lakini sehemu nyingine imekubalika katika marafiki wote. Chokoleti na kadi kibao huhusishwa katika kujaribu kuhakikishiana kuwa penzi bado limewaka moto!
Haya mahusiano ya wapendanao ni sanaa kali sana hasa ukikumbuka tofauti za wanawake na wanaume hata katika kuonyeshana mahaba.
Lakini siku hizi ni kawaida kusikia maswala ya usawa wa jinsia.
Wanaume =wanawake.
Ila kinachonitisha ni kwamba bado katika jamiii utasikia lugha hizi:
Utamsikia mwanamume akimuona mwanadada:Duh !Umeona mtoto yule?
Naamini hamaanishi mtoto mdogo aliyezaliwa, lakini huhisi kwamba kunakauhusiano ndani zaidi ya asemaye hivyo kuwa;
mwanamke = mtoto.
Nasikia vilevile wanawake wanamajinayao kwa wanaume:Buzi, Nguruwe nk
Lakini mimi pamoja ya yote ningependa heshima ikuwe zaidi katika jinsia hizi mbili.Na ningependa wanawake wadhidi kuheshimika. Kumbuka hawa ndio mama zetu. Halafu ni ukweli bado hawapati heshima wastahilio.
Tuachane na mifano hiyo yangu ya juu niliyoitaja. Haina nguvu katika kutafsiri mahusiano ya mwanamume na mwanamke. Labda msome Lisa Melton katika atiko yake ajaribu kuelezea naye jinsi gani wanaume huanza kubadilika tokea SRY gene inapoanza kufanya mambo.
Ila kuna huyu Karen Salmansohn ambaye kunabaadhi ya marafiki zangu wa kike wanampenda sana kwenye kitabu chake aongeacho jinsi ya mwanamke awezavyo kuiga siri za wafundisha mbwa jinsi ya kum-control mwanamume.Anadai kama wanaume watokeavyo Mars, mbwa pia. Kama wanawake watokeavyo Venus, paka pia.
Baadhi ya asemavyo kongoli hapa.
Swali:
Hivi wewe unarafiki wa jinsia tofauti asiyekutamanisha kunanihiii?
Mimi nao.
Je, na wewe unaamini katika jamii huru ni mwanamke awekaye mazingira ya mwanamume kumtupia kauli?
Duh!Nakiri sijui mbinu za utongozaji wa wanawake!
Haya kwa wale washeherekeao Valentine's day.Mmeshanunua machopochopo?
Heri ya Valentine!
Lakini ngojea mimi niendelee na Manu Chao hapa.....
4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Simon: Kumbe unamsikiliza Manu Chao?
Unajua suala la kuwa na rafiki wa jinsia tofauti ambaye ni rafiki tu huwa nalifikiria sana. Ninaudhika sana inapotokea watu kutoamini kuwa inawezekana ukawa na rafiki wa jinsia tofauti bila kuhusisha masuala ya mapenzi. Mtazamo huu ndio hufanya mara nyingi ukitaka kujuana na mtu wa jinsia tofauti anakuwa anaanza kuhisi kuwa labda unamtaka. Kumbe wakati mwingine humfikirii hivyo, unamuona tu kama binadamu mwenzako ambaye ungependa kufahamiana naye.
Urafiki huu unawezekana na una faida zake nyingi sana. Mimi kama mwanaume hakuna sababu eti ya kuwa na marafiki wa kiume tu, na wa kike wawe ni wale ndugu wa damu. Halafu wale ambao sio wa damu nikitaka kuwa na uhusiano nao lazima uwe wa kimapenzi. Dunia hii tunaishi wote, wanawake kwa wanaume. Hakuna ubaya kuwa na mahusiano wa wote, wa kike na wa kiume, bila kuwa na hisia zozote nje ua uhusiano wa kawaida.
Kitururu ww mwanasaikolojia nini?
Anyway umeichambua vzr hii mada. Nikiwatazama wanawake, wengi huwa hawapendi kuwa na urafiki wa kawaida na wanaume kwa kile wanachokiita kutunza heshima zao mbele ya wenzi wao. Lkn naona hili linasababishwa na mfumo dume ambao ndio hasa umeijenga tabia hii miongoni mwa wanawake. Ninao marafiki wa jinsia zote,lkn ilinichukua muda kumuelewesha msichana wangu aina ya urafiki nilionao na wasichana wengine.
Kuhusu siku ya wapendanao nina walakini kama kweli ni siku ya wapendanao. Wapenzi wengi wanaitumia siku hii kuonyeshana kama kweli wanapendana. Mfano, kama kweli unampenda mwenzako ya nini kutumia ndomu? Jibu, hakuna haja. Kutokana na hili siku hii huacha maumivu makubwa miongoni mwa wapendanao ikiwa ni pamoja na maambukizi ya VVU halikadhalika mimba.
Mimi siku zote ni valentine kwangu.
Tchao.
@Ndesanjo: namsikiliza sana Manu Chao.
@Mtanzania: mimi sio mwanasaikolojia. Profesheni yangu ni biashara.
Manu Chao baba lao. Nilikuwa simjui Freddy Macha ndio alinipa kaseti yake mwaka juzi. Moto wa kuotea mbali.
Post a Comment