Mkopo na ladha ya ukwaju!
>> Thursday, February 01, 2007
Katika kipindi nasoma Mazengo Secondary, siwezi kusahau jinsi ilivyokuwa kasheshe pale mkopo wa chapati kwa Mama Kabota ulipokuwa umepitiliza. Halafu unajua huna sababu nyingi zakuombea pesa nyumbani. Kisingizio cha kuugua ulishakitumia ukatumiwa pesa. Iliyobaki unaanza kubadilisha njia ya kukwepa maeneo yote ambayo unahisi utagongana na Mama kabota. Ukigongana naye bila kutarajia unanywea mpaka unajionea huruma mwenyewe.
Kwa ujumla kudaiwa ni jambo ambalo linazingua sana. Unaweza ukastukia umebunia njia za uchochoroni ambazo haujawai kuziwazia ili tu kukwepa kugongana na anaye kudai. Safari ya dakika tano inaweza kukuchukua saa nzima kutokana tu na kumkwepa anayekudai.
Sasa mimi inanishangaza jinsi Viongozi wetu wanavyokuwa huru kwenda kuomba mkopo mwingine. Wananishangaza waonekanavyo wenye furaha na uhuru wawapo pamoja na wanaodai. Halafu hukawi kukuta hata wakiwa likizoni wanaenda kupumzikia kule wanakodaiwa. Hivi hii ni hali ya mkopajia au hili jina mkopo linamaana tofauti kwa viongozi wetu?
Unakumbuka unavyonyong'onyea wakati unaenda kuomba mkopo?Je, huwa unapata kigugumizi eeh!
4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Ya kudaiwa si vizuri. Waweza kuwa mtumwa hasa pale unaposhindwa. Mkuu karibu kwenye kiwanja changu.
Kusto,
Katika makala zako nyingi sana hii ni moja kati ya zile zilizoniacha hoi sana.
Niliongea na Dennis Londo nikamsimulia kuhusu hii akacheka sana.
Kazi nzuri, tuwasiliane,
Ni mimi nduguyo,
MtiMkubwa.
@Mtanzania, asante kwa kunitembelea
@Mtimkubwa, asante Mzee!Duh lakini mkopo nishai!
Post a Comment