Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Unaweza kujivunia Uafrika?

>> Friday, February 16, 2007


Kuna watu wananiambia kuwa mara nyingi inakuwa vigumu kwao kujivunia Uafrika. Mimi siwakatalii, kwani ni ukweli Afrika inamatatizo kibao. Kuna watu wanamatatizo kibao mpaka ingawa ninamatatizo milioni na uchafu huonaaibu kulalamika.

Lakini hebu niseme....


Napenda kurudia kusema kuwa, kwa viongozi wetu wa Afrika nirahisi kujivunia Uafrika kwa sababu wanaufaidi kuliko sisi wengine.
AU?

Lakini ngojea Thabo Mbeki aseme....


Kwa sababu nimemgusia Raisi wa Afrika Kusini, halafu ni ijumaaa, sitaki kukuacha bila muziki. Kwa muda mrefu miziki ya Afrika Kusini imenisaidi kupitisha siku za shida na raha.Wikiendi nyingi nimehuzunika na miziki hii na kufurahi na miziki hii.

Ngoja tujikumbushe historia fupi ya miziki ya Afrika kusini.....


Haya basi!Ijumaa na wikiendi njema!
Doh!Jinsi siku zinavyokimbia mtu utajistukia mwaka umeisha halafu chakuonyesha hakuna!

Swali:
Hivi historia ya miziki ya Tanzania imeshafanyiwa kazi?

Ngoja nikuache na ........


Afrika ndio iko mawazoni leo hii.Je, wewe unajivunia Uafrika?.

8 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Rama Msangi 8:38 am  

nimekuta ujumbe wako kule kwenye blogu ya Jumuiya yetu. Sidhani kama ina tatizo lolote kwakweli au labda ulikuwa unakosea anwani?
- http://msangimdogo.blogspot.com au ikishindikana hiyo basi jaribu
- http://uchambuzi.blogspot.com

Simon Kitururu 8:42 am  

@msangimdogo:hii ya uchambuzi.blogspot.com hua haitatizi. Ni hii ya zamani ya msangimdogo.blogspot.com ndio huwa nashindwa kuingia.Sijui ni kwasababu gani.Labda ni computer yangu na connection inayozingua.

Unknown 1:25 pm  

ujumbe mzuri kwa mwisho wa wiki.kuna aina nyingine ya wale tusiojivunia uafrika ila tunajivunia utanzania.kila mara ninapoitetea Afrika hufanya hivyo kwa sababu Tanzania iko Afrika.

Simon Kitururu 10:03 am  

@Zemrcopolo:hiyo ni kweli tupu!Lakini Zema? Tutafanyaje?

Innocent Kasyate 3:56 pm  

Nimeguswa na mziki wa Tanzania; manake siku hizi ni Bongo Fleva. Mie binafsi napenda sana mambo ya kina Msondo, Sikinde, Pamba Moto, Sendema. Ila hizi hazipigwi redioni.
Kuna bwana mmoja wa Mwanza anaitwa LUSUNGU, anatangazia Free Africa FM, kweli jamaa anajaribu kuuenzi mziki halisi wa Tanzania.
Binafsi niseme najivunia uafrika japo nadhani ipo kazi kuzuia kumezwa kwa utamaduni wetu na kusahaulika kabisa.

luihamu 5:01 pm  

Mimi najivunia rangi yangu katika ardhi yangu,nipo katika ardhi ya mtu mweusi,labda niwaulize, JE MNAJIVUNIA UAFRIKA?

Simon Kitururu 10:41 am  

@Luihamu:Unamaanisha nini?

Simon Kitururu 2:27 pm  

@Innocent!ulichosema kweli tupu!lkini sijakuona hapa muda mrefu sana Inno. Nitembelee mara kwa mara. Mimi kwako nakutembelea sana!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP