Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UKOKO!

>> Friday, February 23, 2007


Ushawahi kuwa shabiki wa ukoko? Utandu je? Bwana eeh!Kuna wakati nilishajenga tabia ya asubuhi kukwepa mikate na vitu vingine na kuhakikisha napata kiporo cha wali na maharage ya nazi ya jana. Hasa yale yasio na rojo sana. Basi hapo nikipata na chai basi siku imeanza.

Lakini ngojea turudi kwenye Pizza. Nisisahau na hambaga. Unajua hivi vyote ni vyakula vya walalahoi vilivyowafanya baadhi ya watu kuwa mamilionea.Sasa bongo tuna vyakula vingapi vya walalahoi hatujavifanyia kazi?.Au tunasubiri tuone mpaka Malkia akivitafuna, kama Pizza ilivyopata umaarufu ndio tuvishabikie?
Usitishike najiuliza tu!
Tuendeleze libeneke.

Namuachia stereoman..

10 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Kibunango 12:50 pm  

Kwa Tanzania nafikili Ugali ndio chakula maarufu. Ugali kwa upande wa Visiwani ulichukuwa muda mrefu kuzoeleka, wao wanapenda kuuita Sembe!
Pale Forodhani kuna Pizza ambayo ni tofauti kabisa na pizza za kawaida, Hata hivyo wamekosa jina muafaka kwa pizza hiyo na wanaiita Zanzibar Pizza...

Simon Kitururu 12:59 pm  

Ugali ni maarufu sehemu kubwa Tanzania.Kuna sehemu nasikia wakila wali hawashibi. Lakini mimi kwa sababu sijui nilikuwa naenda sana Kyela wakati niko mdogo nikajikuta nimezoea wali kuliko Ugali

MTANZANIA. 4:04 pm  

Kitururu!
Hongera sana kwa staili yako ya ku-blog hasa namna unavyochagiza kama si kuchombeza kwa muziki.

Kaka katika jamii ninayotoka bongo, chakula chetu kikubwa ni ugali-kilugha ni "WA'RI". Mara nyingi unalika sambamba na maziwa na nyama bila kusahau mbogamboga.

Lkn bwana ugali huohuo nilipokuwa sekondari ya bweni niliukinai vibaya. Kule unaitwa bondo,nguna n.k.

Kwa ufupi vyakula vyetu bongo ni ugali,ndizi, kande n.k

Simon Kitururu 5:05 pm  

@Mtanzania: kabila gani hilo wanaita ugali Wari?Lakini bwana sidhani kama kuna mtu ana kula ugali shuleni !Kila mtu nafikiri inakuwa bondo!W ashuleni, utamu wake haufananai na ugali ingawa unaitwa ugali.

Jaduong Metty 5:25 pm  

Simon,
Kwangu bwana utando ndo zaidi. Wali wa nazi ukipaliwa na mkaa, halafu ukawa na utando fulani hivi "crunchy", basi hiyo kitu usiseme. Haswa unapokuwa bado wa moto.

luihamu 5:51 pm  

Mzee Simon umenikumbusaha mbali sana,nakumbuka kipindi nikiwa morogoro nilipenda sana kula ukoko wa wali au ugali.Duh mbali eh.

MTANZANIA. 6:19 pm  

Kitururu!
Hao ni "WARANGI" toka wilayani Kondoa mkoani Dodoma.
Kwa kirangi "wali" ni "wali" ila "ugali" ni "wari" au "warii"

MTANZANIA. 8:17 pm  

Simon! Samahani nipo nje ya mada kidogo.Kama unafahamu huu wimbo una maana gani?http://www.youtube.com/watch?v=itzTgp39NaY
Madilu anaimba kwa hisia kweli halafu hayati mzee mzima anachombeza kwa ustadi mkubwa. Ni hayo tu

Simon Kitururu 9:58 am  

@Mtanzania:sielewi anasema nini. Lakini ni ukweli anaimba kwa hisia sana.Labda Mtimkubwa akipita hapa atatusaidia maana ya wimbo huu.

Simon Kitururu 12:36 pm  

@Metty: karibu sana kijiweni! Ushajaribu kutumia makaa ya grill hapo chobisi? Kuna jamaa huupatia utando kiaina.Mimi huanasubiri mpaka bongo ndio nawaachia wajuzi.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP