Ukiniuliza kuhusu Tanzania vitani!
>> Tuesday, February 27, 2007
Ukimsoma H.G Wells katika kitabu chake cha The war of the worlds, unaweza kufikiria kuwa ni mpaka vibwengo kutoka sayari nyingine waingiapo duniani ndio vita kabambe inaweza kutokea. Ukifuatilia jinsi vita mbalimbali, sehemu mbalimbali duniani vilivyoweza kutokea hata zile sehemu watu walipoonekana kuwa wanaishi kwa amani,Tanzania chini ya uongozi mzuri tunaweza kuanza kupigana vita wenyewe kwa wenyewe. Ukifuatilia Bosnia miaka ya tisini, Ujerumani miaka ya thelathini, bila kuwasahau Watusi na Wahutu , hapo jirani, lolote laweza kutokea Tanzania.
Kinachohitajika ilikufanikisha vita Tanzania ni uongozi bora.
Au ulitaka niseme uongozi mbaya?
..lakini tuendelee na sababu zinazoweza kuondoa amani....
Kusahau ladha ya utamu wa amani .Uchumi kuendelea kudidimia wakati viongozi kuendelea kunawili.
Duh!
Dini nazo zikiendelea kutuaminisha maswala na kutusahaulisha kutumia akili.Akili nazo zikiendelea kukosa chakula kiiakikishiayo makali yasaidiayo kutatua matatizo yatukabiliayo, na hata pia kushindwa kututuliza katika dakika ambazo maamuzi lazima yatolewe.
Tanzania pamoja na yote ni jamii iliyogawanyika ingawa mara nyingi tunapenda kubisha. Ni rahisi sana kugundua kuwa:
- Ukabila tunao
- Udini tunao
- Umasikini tunao
- Uongozi bora ambao unaendelea kutufanya masikini tunao
- Mfumo wa kisiasa ambao haujatengemaa tunao
- Ujinga tunao
- na nakadhalika tunayo.
Lakini vilevile naamini tunamatumaini. Hakuna haja ya kukata tamaa.
AU UNASEMAJE?
2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Simon nafurahishwa na jinsi unavyotafakari kuhusu Tanzania.dakika chache zilizopita nimeongea na jamaa yangu aliyeko uholanzi kwa kozi fupi.yeye na wenzake wanalaani watanzania wanaokaa nje.nilichomwambia ni kwamba amshukuru mungu kama kwake yeye kukaa Tanzania kumemuwezesha kutimiza ndoto zake.nadhani itabidi nimfowardie blog yako ili kumuhakikishia kuna watanzania ughaibuni wanaowaza Tanzania siku zote.
Mzee Zemarcopolo, Mwenzio sina ujanja kwahili.Vigumu kusahau Nyumbani. Halafu mara nyingine ukiondoka sehemu unakuwa na uwezo wakuamngalia ulikotokea kwa jicho la pembeni.
Post a Comment