Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

ASANTE TOTO JINGA KWA KUTOENDA SHULE!

>> Thursday, September 20, 2007

Swali:
Unajua unaweza kujua zaidi kutokana na kutofundishwa?

Wanadamu maishani ni wanafunzi.
Unaweza kumlaumu mtu kwa kitu ambacho wewe mwenyewe ulijifunza kwa kubahatisha, kutokana na nafasi uliyokuwa nayo kama mtoto wa mganga wa kienyeji.

Lakiniiiii.......

Kujua mizizi fulani na jinsi ya kupaa na ungo, ilikuchukua muda.

Kumfikisha kilele mtu.......,

....... cha kumdanganya, kumuambia ukweli,....... kimapenzi,.....
ndio kabisaaaaaa,..... ukibadili mtu, nukta za utamu unaendelea kujifunza upya.

Swali:

  • Ushastukia! Kumdanganya mtu, saa nyingine inabidi ubadili jinsi ya kudanganya?
  • Au, unaamini wanasiasa kutokana na kufanikiwa kwao kwa kutumia uongo uleule?

Kutokwenda shule, sioni ni ujinga mara nyingine!

Nashuhudia wasomi wanavyofanikiwa kufanya vizuri ujinga baada ya kwenda shule.
Wengi wanaotundika vyeti vyao sebuleni, ni kweli wameenda shule.

ILA.......


Tatizo la kwenda shule , ni kipimo chake!
Kipimo chake, ni cheti´chake , ambacho aliyeamua ndio kiwe kipimo, ndio mjanja, na aliye elimika.

Swali:
Shule ni nini?

Shule zetu za jando na kutairi wanadada, zilikuwa bomba.
Zilitufundisha jinsi ya kuishi katika mzani wa nani anaamua na nani anaitikia.


Kwa mwanamume, ilikuwa uroda sana katika tamaduni nyingi, kutokana na uwezo wao wakuamua kucheza bao, wakati mwanadada anakuchemshia maji yako ya kuoga nyumbani, na ile minofu ya nyama iliyonona, watoto wako wanakatazwa kuigusa, unaahifadhiwa.
(sijui kwanini naongea swala hili katika tensi iliyopita!)

Swali:
Hivi unafikiri Mwalimu wa kwanza duniani alikwenda shule gani?


DUH!


Ushastukia!

Mwalimu wako wa dini, si lazima alikuwa anajua jinsi ya kumloga nanihii....?

AU?

Shule ni kitu cha ajabu.
Kwa sababu ni kitu kigumu kiasi watu fulani wakaamua kurahisisha na kujenga majengo ili uweze kunyosha kidole nakusema; nilienda shule ileeee!

Shule kiboko , kwa sababu inaweza kukukaririsha vitabu kibao ambavyo utajisifia sana unapofanikiwa kufaulu mitihani fulani, na katika kikundi, kuonekana mkariri fulani, samahani, kuonekana unaakili.
(Samahani lakini kwa kukutambulisha! Nilikua sifeli darasani.Ila baada ya kulijua darasa nikastukia nafeli kila siku. DUH!)

Swali:
Shule ni nini?

Darasa je?

Ushastukia shule fulani, zinafanya watu fulani wajisikie kufakufa?

Samahani!

Siongelei shule za kidini hapa za kujilipua, ambazo nyingine Bin Laden Alifeli.

Si unajua tena!

Bin Laden hajajiua, ingawa wafuasi kadhaa wamefanikiwa kuji ......

Duh!


Naongelea shule hasa za kujiua ukishachoka kuwa hapa duniani sasa hivi.

Ukijisikia kufakufa, unaweza ku google shule hizi na kufundishwa.

Naamini unajua kuwa utakuwa unajiua ukifuata hizo shule ,kitu ambacho nitakushangaa kama unauhakika kuwa ni jambo la busara.

Swali:
Hivi kwanini watu wanajinyonga wakati kuna njia rahisi za kujiua?


Samahani kwa wote ambao darasa linachukua kitu kikubwa katika kujijua, mpaka hauwezi kua Zubeda au Halufani bila kujitambulisha kwa cheti fulani!

Lakini najua kuwa Marconi aliyerusha matangazo ya kwanza kutoka bara moja mpaka jingine, alikuwa mjinga darasani.

Namkumbuka Leornado Da Vinci, alikuwa mjinga katika wasomi waliokuwapo enzi zake.

Watu wameenda shule bwana!

Naweza kuwaongelea wengi kama akiana Albert Einstein ,bila kumsahau.....aliyegundua kujisaidia porini.


Duh!




Ningekuwa siwaogopi , ningewauliza shule Yesu na Mohamedi walizoenda.
Lakini najua hawa .....nitakua nimeenda mbali .
Si unajua
,ni vigumu kuelezea mahusiano yao na Mungu au Umungu wao
?


Metty najua wewe mdini:-)

Swali :
Hivi Mkwawa ,Zulu fulani na .........walienda shule gani?

Duh!

Nimeacha!
Samahani!

Lakini...

Shule au sio shule , wote tunatafuta kujazia kakitu fulani .
Kujazia kale kasehemu ambako kwa sababu sisi ni binadamu, hakazibiki.
Mzani tu ndio unaegemea upande ambao kaubongo kakibinadamu kanatuambia kunaupungufu.

Swali:
Si unajua ubongo unaweza kukushauri uchambe kwa maji kwa sababu makokoneo ya karatasi huacha vimavi fulani?


Duh!

Tulia na OSIBISA watukumbushe miaka ya sabini jinsi bendi za Afrika zilivyokuwa na wanamziki bomba.

DUH!
Najua wanamziki bomba kutoka Afrika wanatawala na miziki bomba sasa hivi pia:-)


0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP