Saikolojia Ya Kuzoea Kuonewa!
>> Saturday, September 01, 2007
Ukionewa sana, kuna hatari ya kuzoea kuonewa.
Ukionewa sana kuna kastarehe kake kakupako uhuru wa:
- Kulalamika unaonewa.
- Kupata watu wengine kukuonea huruma kitu ambacho kinawafanya wajisikie vizuri kuwa wao mambo yao hayajaharibika kama yako.
- Kutokuwa na sababu ya kujilaumu kwanini umeshindwa kutokana na ukweli una kisingizio unaonewa.
Swali:
- Ushastukia kuwa kale kakitu watu wapiganiako sana, mara nyingi wakipewa wengi wanasahau umuhimu wake?
- Unakumbuka kuwa watu weusi Marekani, waliwahi kupigania haki ya kupiga kura , lakini mpaka sasa wengi wao wanabembelezwa mpaka na akina P.Diddy waende kupiga kura?
- Unajua kulalamikia uonezi kunahitaji ujuzi na mazoezi ingawa tukizaliwa tu tunaanza kulalamika?
Lakini kuonewa kunahitaji kujua haki yako ni ipi.
Naamini kuwa katika nchi kama Tanzania ambayo haki zetu wenyewe, wengi wetu hatuzijui, kuonewa kwetu ndio kwanza tunakustukia.
Nakubali , binadamu anaakili na mambo mengi ayahitajio anakuwa anayajua tokea akizaliwa tu.
Lakini....
Tatizo la binadamu ni uwezo wake wakustukia na kujiongezea ayatakayo. Na akijiongezea ayatakayo na akijua kuwa hakuna kipingamizi kwake kuyapata ,ndio hapo basi na nafasi ya maonezi inapokua pia, kwa sababu kuna binadamu wengine wanasilika yakutaka kukunyima na kukuonea, kwasababu wanataka kukunyima na kukuonea tu ingawa kakitu wakunyimako au wakatumiako kama kadude kakukuonea, hakawasaidii kitu wao binafsi.
Duh!
Swali:
- Umezoea kuonewa?
- Au ujastukia unaonewa?
Tatizo malalamiko mara nyingi hayatatui maswala bila kuchukua hatua ya vitendo.
- Si unajua dua la kuku halimpati mwewe?
Ngojea Gwiji niliheshimulo katika Tarumbeta, Miles Davis akukumbushe Human Nature nafikiri unaukumbuka ule wimbo wa Michael Jackson.
6 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Eti Simon!
"...kuna binadamu wengine wanasilika yakutaka kukunyima na kukuonea, kwasababu wanataka kukunyima na kukuonea tu ingawa kakitu wakunyimako au wakatumiako kama kadude kakukuonea, hakawasaidii kitu wao binafsi."
Nani amekuonea kiasi hichi unalalamika usiku kutwa?
Kisha tena...Miles Davies...rush, rush umenikumbusha kitu kingine ...
yeah, ni kweli kuna wengi wanafikiria wanaonewa...sidhani wana hujua wanaonewa wakizaliwa.
Duh Katibu,haki tuache kulalamika lakini tutaachaje kulalamika wakati.......
akina P.Diddy waende kupiga kura?..
i told yah o was learnin..is this somethin to do with P.DIDDY voting?..
men?..am comin there...
@Kisiki:Si utani!
@Rasta Luihamu:-)
@It is true it is about voting. I was talking about how he was trying to mobilize people to go and vote.The sad part is that, when blacks were not allowed to vote, they started fighting for that right.Now when they have voting right, a reasonable part of the population avoid voting.
Post a Comment