Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

USHASTUKIA !KIPINDUPINDU HUWARUKA VICHAA WALAO MAJALALANI.

>> Friday, September 14, 2007

Watu hukimbilia kusema kuwa Mungu anawalinda watu fulani, ndio maana hawapati kuharisha.

Mimi nafikiri kuna kitu zaidi ya hicho.

Naamini mwili wa binadamu unamambo yake. Mwili wako na wangu vinafanana jina tu. Wewe kama umekwepeshwa kukutana na uchafu fulani, mwili wako ukajifunza kupigana na vichina viletwavyo na uchafu huo, tunaweza tukashea sinia la ubwabwa lakini wewe ndio utakaye tembelea msalani mara kadhaa kwa tatizo la kuumwa tumbo au geti la haja kubwa kutokubali kufungwa kwa idhini yako.
Vichina , samahani virusi, vinaenda gym kila siku , hivyo kama mwili wako haujengi misuli ya kujikinga na virusi hivi, jasho litakutoka.

Kwa bahati mbaya baadhi ya misuli katika mwili wako inatokana na ulivyorithi kutoka katika kizazi chako. Kama kizazi chako hakikujenga kinga zitokanazo na mutation mbalimbali ndani ya mwili wako zikulindazo, ukicheza
peku hovyo, lazima UKIMWI ukuondoe.

DUH!
Sasaaaa....ngojea turudi kwa kichaa......

K
aribu katika kila miji kibao, katika nchi zinazoitwa zinaendelea, kulikuwa au kuna kichaa fulani maarufu mjini.Tanzania ni miongoni mwa nchi hizo.

Swala hili tunaweza kushukuru serikali na jamii yetu nzima kwa jinsi ilivyofanikiwa kuwaacha ndugu na jamaa mtaani , baada ya kurukwa na akili.


Kwa kuwa jamii zetu zimefanikiwa pia kuacha majalala na uchafu kibao mtaani, mara kwa mara tumefanikiwa kutembelewa na ugonjwa wa kipindupindu mtaani. Inatambulika kuwa vijidudu vya kipindupindu hupenda kuishi katika sehemu chafu ,kama majalala watu watupapo makombo.

Kwa bahati mbaya huku majalalani pia vichaa hupapitia sana kufuatilia makombo ya vyakula kutokana na jamii kutofanikiwa kuwalisha. Hata wasipokula jalalani , ni makombo ya vyakula yaliyochezewa ngwasuma na nzi, ndio waambuliayo mara kwa mara.

Swali:
Sasa mbona kipindupindu kikija hawajamaa kinawakwepa na kumdaka jamaa anayekunywa maji yasiyochemshwa?(Labda ni seme maji yenye vijidudu , kwa maana kuna nchi kibao nimekatiza, maji yao ya bomba au yasiyochemshwa ni salama tu..)

Sasaaa......
Tukitoka kwenye sebule ya Kipindupindu na kuingia chumbani kwenye UKIMWI.........


Swali:
Je , unafikiri gonjwa kama UKIMWI linawapata watu wote baada ya kucheza mchezo wa baba na mama?

Duh!
Hata sihitaji kusema sana kwa hili. Ila nachojua ni.......

Dunia ina mwisho, lakini kuna watu wagumu kuiondoka dunia hii kwa yale tuliyo nauhakika ndio yatuuayo.

Imeshagundulika hata Nairobi kuna wadada hawashikwi na mdudu ingawa wanacheza kiwanja chenye mdudu.
Soma hapa.
Au turudi nyuma kidogo kwenye kastori haka, kalikotokea nchi kadhaa wa kadhaa duniani.

DUH!

Najaribu kusema kuwa, kila mtu na kila siku tunaijenga miili yetu kinamna tofauti. Miili yetu inakinga tofauti kutokana na mabadiliko yatokeayo ndani ya mwili kutokana na tunayo kutananayo kila siku.

Sasa maswala ya mutation ya CCR5 genes au delta 32 yanaonyesha jinsi gani baadhi ya watu wanaepuka magonjwa fulani kama UKIMWI.[Nisikutishe sijui sana maswala ya genetics:-)]

Mimi naamini.....
Mimi na wewe kunakitu kizazi chetu kiliepuka ndio maana bado tunaendeleza libeneke leo hii.
Lakini kumbuka sisi ndio tunaweza kuwa hitimisho la kizazi ingawa kizazi cha Ze Zubeda kikawa kina dunda kwa miaka maelfu fulani yajayo.

Duh!
Mara nyingine kukwepa sana kitu ni kujidhoofisha.Lakini kumbuka ukikumbwa na kabingwa fulani kama UKIMWI , hauna nafasi kubwa ya kupitisha zile jinsi zako kwa kizazi kijacho.

Kumbuka sehemu karibu zote duniani, bado hawahifadhi mbegu za kiume na washikaji zake, unajua tena, wale mayai ya kike ya binadamu yalioathiriwa na vichina vya UKIMWI kwa aajili ya taifa la kesho litakalo jua zaidi jinsi ya kuutekenya udhaifu huu wa UKIMWI na kadhalika kadhaa zitusumbuazo hivi sasa, halafu jamii ikacheka.

DUH!
Usitishike wote tutakufa!
Lakini cheza salama.

WIKI MWISHO NJEMA!
Burudika na Rikki Jai akija na miondoko ya Soca Chutney


6 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Anonymous 5:51 pm  

Aisee njia yako ya kufikisha ujumbe ni bomba ile mbaya (NZURI) Mtu akisoma mada zako ni lazima akutane na KICHEKESHO, halafu anapata UJUMBE. Big up saaana

Simon Kitururu 4:32 am  

@Said:Asante kwa kunielewa.

Anonymous 11:17 am  

Duh!

Simon Kitururu 6:49 pm  

@Exceess:-)

KKMie 1:58 am  

Leo nimefanikiwa kuingia bila kiduduz, ila nimecheka sana nakuelimika as always.

Duh! Kazi nzuri Simon...

Simon Kitururu 3:52 am  

@Dinah:Asante!Najaribu kuondoa , kiduduz hakijaisha lakinni.Kuna mdau ananisaidia kuwapulizia sumu.Karibu sana!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP