UTAMU WA KUFANYA DHAMBI!
>> Tuesday, September 04, 2007
Watu wengi ingawa hawatakiri hadharani, hupenda kutenda wakatazwayo.
Wapo wengi wafurahio kuvunja sheria kwa sababu tu zimeitwa sheria.
Swali:
Unafikiri kwanini kuna sheria?
Ukikatazwa kudokoa mboga, halafu ukajikuta pekee jikoni mbele ya sufuria fulani , mdadi wa kudokoa unaweza kukupanda.
AU?
Ila, kumbuka kama hujakatazwa kudokoa mboga, ukajikuta jikoni mbele ya sufuria fulani , unaweza ukaonja hiyo mboga na utandu, na wote tukaamini kuwa umeonja mboga na hukudokoa.
Nilipokuwa nafuatilia maswala ya kwanini watu kupenda kula uroda pekupeku hata kama wanajua kuna UKIMWI, nikastuka kupata data zionyeshazo kuwa watalii wengi kutoka nchi za ulaya kaskazini , wasafirio kwa ajili ya kutafuta uroda(sex tourism), mara nyingi hulipia ngono kwa bei ya kuvaa soksi lakini kisiri katika shughuli huibia na kuvua soksi.
Si unajua tena pekupeku bei yake ni ghali kuliko na soksi. Kisa cha wengi kuvua soksi kisiri wakiwa kiwanjani , ni kujaribu kukomesha au kuvunja sheria, kwasababu wameambiwa na mwanadada lazima wavae soksi kwani anaogopa magonjwa au atapandisha bei. Kitu kama hiki ambacho chaweza kutafsiriwa kama cha kijinga, kinatokea tu kutokana na silika ya baadhi ya watu ya kuvunja sheria.
Nakubali lakini wapo wavuao soksi au kutovaa kabisa soksi kwasababu wanasema wakivaa soksi chakula hakinogi.
Swali:
Ushawahi kukatiza katika uchochoro ambao umebandikwa kibao kisemacho;ni marufuku kupita hapa?
Duh!
Turudi kwenye dhambi......
Nakumbuka unakumbuka kuwa karibu dini zote zina jaribu sana kutukaza kufanya vitu fulani kwa sababu ni dhambi.
Dhambi inasemekani ni mbaya sana.
Tatizo la dhambi ni kautamu kake, hata katika dini zetu , dhambi hizi utamu kunoga, zimeelezewa kinamna ambayo inaonyesha ni vigumu sana kuzikwepa. Lakini nahisi watu wengi wanajizuia kufanya dhambi kutokana na hofu ya baada ya kufa watajibu nini kuhusu madhambi waliyokuwa wanashabikia pale chobisi.
Chakutisha ni kwamba dhambi zinazoeleka.
Ndio maana unakuta wahubiri wa dini karibu zote, ukiwafuatilia, utakuta kunatudhambi wanatufanya kwa bidii tu.
Tudhambi twa:
- ngono nje ya ndoa,
- kuiba sadaka,
- kugombanisha waumini
- kudanganya
- kuua kwa jina la dini au Mungu
- ku...
- nk.
Lakini tukumbuke...
- Ukifanya dhambi mara ya kumi , kuna tofauti na ile ya kwanza.
- Dhambi uirudiayo mara ya ishirini, haikutesi katika dhamira kama ile ya kwanza ya kumchungulia nanihino akioga.
Swali:
Ushastukia kale kadhambi utendako, ambako kako kwenye dhamira, kale usikotaka kukafikiria sana?
Usitishike !
Ni siri yako hiyo, sisi hatujui!
Na sisi wote tuna dhambi, ingawa nasikia binadamu wengine wameshinda lotto yakuitwa watakatifu.
DUH!
TUTUBU LAKINI!
Kumbuka :
- Dini nyingine zinasema dhambi za kukusudia hautasamehewa. Kwahiyo kama umeshazifanya na kuzirudia mara kenda na uche...Jehanamu inaweza ikawa inasubiri.
- Sina uhakika kama ukihama hiyo dini ikutiayo hatiani sasa na kwenda katika ile isemayo utasamehewa, kama utaponyeka.
Duh!
NAACHA BASI!
Tutulie na nyepesi nyepesi kutoka Japan ihusuyo doli liitwalo Kuma kama iletwavyo na Hikaru Utada , katika wimbo boku wa kuma
6 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
tupo pamoja kaka
Mada zako zimeenda shule si mchezo! napenda sana kusoma, kuuliza na lusikiliza MASWALI kuyajibu ndio ngoma. Endelea kushusha nondo za kufa mtu MKUU!
Ni kweli dhambi nitamu lakini ina madhara chungu nzima...tuchague gani?
@Chemshabongo:Poa Mkuu!
@Said:Kuuliza maswali ni kweli ni rahisi kuyajibu hapo ndio kasheshe.
@Kisiki:Nahisi hata kuchagua dhambi, mara nyingi tunakatazwa!Kazi kwelikweli!
Simon vipi kaka?
Huwa napita hapa fasta, bila kuacha maoni ila tupo wote.
Nitatulia ulingoni hivi karibuni na hivyo lile swali lako nitalijibu.
Haya maswali yako yananifikirisha sana mtu wangu.
@Bwaya:Tuko Pamoja Mkuu!Nilikuwa najiuliza umepotelea wapi?Nakusubiri urudi ulingoni.
Post a Comment