KUIVA ni MWANZO wa KUOZA kwa TUNDA!
>> Friday, September 21, 2007
Wengi wetu hufurahia tunda likiiva.
Tatizo la tunda likishaiva, ni muelekeo wake.
Lakini....
Tunda likiiva , hatua inayofuata ni kuiva sana, halafu kuoza.
Tunda lililooza wengi tunalikwepa ingawa ndio mimba ya mbegu zitubarikizo na mimea kedekede.
- Kuiva ni kufikia katika kikomo cha kipengele.
Halafu wanaostukia wanaweza wasiwe na uhakika na ulipofikia, kutokana na kukumbuka yale wayahusianisho na kipindi mambo yako yalipoiva.
- Kuiva ni kufikia mwisho wa ngazi.
Duh!
Ukifikia ngazi ya mwisho ,unaweza ukapaa, kama unamabawa au helkopta ya kukuchukua hapo ngazini na kukupaisha juu zaidi ya jengo ambalo kiurefu huzidi ngazi.
WIKI MWISHO NJEMA!
Burudika na Mr Nice
2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Yaani unajaribu kutuambia kuwa wachanga(wabichi) kukakua (pevuka) alafu tukakomaa(iva) na sasa tumezeeka(kuoza) na tukisha zeeka ndio mwanzo wa wengine kuja (mmea wa tunda kuota).
Hakika makunyanzi yakianza usoni watu huongeza kasi yakufanya mambo iwe ni kujenga, kungonoka, kuzaa na kuwa karibu na ndugu, jamaa na marafiki.
To be honest sijui naongelea nini hapa hahahahahaha!
Si, kazi nzuri keep it tight!
@Dinah!Duh! Lol!Unatabia,baya ya kunielewa weee. Unikomeeee..!Hahaha!LMAO!
Post a Comment