Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UNAWEZA KUPIGA NDEGE WAWILI KWA JIWE MOJA.

>> Saturday, September 15, 2007

Ukilenga ndege mmoja na kupiga wawili, kumbuka umepiga wawili tu na sio wote.

DUH!

Najaribu kusema....

Jambo moja ulifanyalo ,laweza kuwakilisha mambo mawili.

Unaweza kuongea ujinga na hekima katika sentensi moja.

Inawezekana ukiambiwa unaongea busara , ni kwasababu wasikilizaji hawajastukia jambo la pili liwakilishwalo katika hiyo busara , ambalo ni ujinga .

Swali:
Hekima na busara ni nini?

DUH!

Lakini ukipiga ndege wawili maana yake hujapiga wote, ila, kama ndege wawili ndio waliopo, basi unaweza ukawa umepiga ndege wote.

DUH!

Hii ni makala moja, lakini inaweza ikawa inawakilisha mambo mawili.
Umestukia eeh?

JUMAMOSI NJEMA!
Nakuacha na baadhi ya picha za jana baada ya kazi!

Powered by www.myfabrik.com


Tulia na Portishead wakikupa kile kibao kiitwacho Kiboksi cha Utukufu.

10 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Ansbert Ngurumo 12:09 am  

Ndugu,
Blog yako inavutia. Pia umeweka maswali ya msingi. Nadhani yanatafakarisha wasomaji, hasa wanaopenda vitu makini. Hongera.

Simon Kitururu 2:17 pm  

@Ansbert:Asante Mkuu!Karibu sana kijiweni

mwandani 3:10 pm  

filosofia kali mzee. endelea kunifikirisha

Aliko 4:54 pm  

My cents on the Black and white pics zimetoka bomba.. chief ^ mwandani vipi mambo kamanda.

Simon Kitururu 10:41 pm  

@Aliko:Nitakutumia zile picha.Tuko Pamoja!

Simon Kitururu 12:44 pm  

@Mwandani:Tuko Pamoja Mkuu!

Anonymous 6:51 am  

Ebwana eeh! BLOG imetulia mpaka mada zako Mkuu. Endeleza Game

Simon Kitururu 9:10 pm  

@Said.Asante!Tuko pamoja!

Anonymous 4:40 pm  

Nice blogg Simon! big up!
Beah Cannut

Simon Kitururu 5:27 pm  

@Beah:
Asante Mkuu!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP