Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Robert Mugabe VS Askofu PIUS NCUBE

>> Wednesday, September 12, 2007

Inajulikana kila binadamu ana udhaifu wake.
Na watu wakikufuatilia sana watakudaka katika kaudhaifu kako.
Inawezekana kaudhaifu kakawa ni kale kakulialia haraka mambo yakiwa magumu .Lakini kaudhaifu kanaweza pia kakawa ni kale kanakokupa sura tofauti na ile watu waijuayo kuhusu wewe.

Naona Askofu Pius Ncube, akina Mugabe walimstukia kaudhaifu kake ka ngono.
Ingawa anatakiwa awehajihusishi na maswala ya uroda hasa yeye kama Askofu wa kanisa la kikatoliki inasemeka alifanikiwa kujifariji kama wafanyavyo maaskofu na mapadre wengi tu .
Inasemekana lakini kuwa huyu Askofu alikuwa amespeshalaizi kwa wake za watu.

DUH!

Sasa haya ni mambo binafsi.
Hayatuhusu.

Lakini nimejikuta niko katika majadiliano na wadau ambao wamesisitiza kuwa huyu Askofu kama alikuwa anauwezo wakutomuogopa Mungu amuubiriyo na kuwa muongo na Mzinzi, inaawezekana hana tofauti na Mugabe ambaye amezidiwa utamu wa kuwa na nguvu.Hii hoja imetokana na baadhi ya watu kufikiria kuwa ni afadhali ahamie kwenye siasa baada ya kuenguliwa na Papa.

Najua jamaa wamempatia kasehemu kakumkata nguvu za kumpinga Mugabe kwa kuonyesha kuwa ni muongo na mdhaifu kama binadamu wengine.
Lakini haka kamchezo wakianza kukafuatilia bongo si itakuwa balaa?
Swali:
Si Bongo siasa inatafsiri sawasawa na uongo?

Tulia na Boney M

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP