Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UMEDINDA?

>> Saturday, September 29, 2007

  • Tatizo la kudindisha, ni kupooza, baada ya ujanja kufikiwa au kutofikiwa.
DUH!

Mheshimiwa Mwalimu Nyerere alidindisha na UJAMAA na CCM, mpaka baadaye kidogo .

AU?

Baadaye kidogo, akamruhusu Mheshimiwa MREMA avae raba , na wengine kadhaa waanzishe NGO KINYUME, ziitwazo VYAMA vya UPINZANI!

Inasemekana , hata Mheshimiwa Mandela, baada ya kudindisha kwa miaka kibao , sasa hivi ame.........

Duh!

Matatizo ya kushindwa kudindisha, yana dawa ndogo ndogo, kama VIAGRA.

Swali:
  • Nani kasema kuna mtu anashindwa kudinda?
  • Akishindwa ni tatizo?
Lakini......

Tatizo la dawa hizi zisaidiazo au kuongezea urefu wa kudinda, zinamsaada usiodumu kama nguvu zako za kuguna.

Huwezi kuguna muda wote.
AU?

Piga ua,..
...siku moja tu , hata usipo jitahidi kuikwepa..
itafikika, ambayo, nguvu ya kusimamia jambo uliaminilo kutoka chini na juu ya moyo wako, utaamua kulikodolea macho tu, kulaumu na kuguna kisirisiri, kutokana na MDINDO kusinyaa.

DUH!

Nisikutishe!

LAKINI KUMBUKA WEWE, MIMI NA Binti HALUFANI, NI BINADAMU TU!

Huwezi kufanikisha mambo yote.

AU unafikiri KAMBONA na NYERERE, wote wangefanikiwa katika muda mmoja kufika pale........., wewe unge....

DUH!

Naacha!

Pata wimbo wa Kevin Lyttle abadili somo.




6 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

luihamu 2:58 pm  

Mzee Simon(KATIBU)wakati mwingine nashindwa kukuelewa,ninamaanisha nashindwa kuelewa nini unataka kusema,jamii itaelewa kweli unachotoka kuelezea?

Simon Kitururu 3:07 pm  

@Rasta: Kweli hicho kitu!

Mara nyingine hata sijui kama naeleweka:-(

Niko mawazoni tu RASTA!

Naamini nisipoeleweka , Mtu anyoshe kidole tu. Unajua siandiki kama Mwalimu HAMZA alivyotufundisha uandishi! Haya matatizo au faida zakutoeleweka nafikiri zitajitokeza.
ULIKUWA UNAMuELEWA YESU?

luihamu 3:46 pm  

HAPANA MAFUNDISHO YAKE YALIKUWA NA TAFSIRI YA NDANI,INABIDI UWE NA UPEO WA KUTANZAMA MBALI.

Simon Kitururu 5:08 pm  

@Kutazama mbali ndio tatizo. Siunajua uwezo wa macho yetu kuona?

Egidio Ndabagoye 8:29 pm  

Heshima mbele,
Inabidi nitazame kwa jicho la tatu au nitumie kiona mbali.

Simon Kitururu 1:11 am  

@Egdio:Tatizo ni kujua jicho la tatu liko wapi.
DUH!
Kazi kwelikweli!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP