KWA Jalala AFRIKA, NAJUA WEWE SI BIKIRA!
>> Thursday, September 06, 2007
Afrika imekuwa ni sehemu ambayo mataifa mengine yanailenga kuleta uchafu wao ambao wanaona si vizuri kuwa nao nchini mwao.
Mimi binafsi , natishika sana na tamaa za pesa ambazo zimesababisha viongozi wetu Afrika kuruhusu mataifa mengine kugeuza Afrika kuwa jalala.
Kidonda hiki kimefumuliwa na taarifa zilizojaa katika vyombo vya habari zionyeshazo jinsi gani mataifa mengi duniani yanarudisha mali zilizotengenezwa China huko huko Uchina kutokana na kuwa na sumu na pia kasoro chungu mbovu.
Nafikiri kama wewe ni mfuatiliaji wa habari, utastukia katika miezi hii michache, kuanzia vyakula mpaka madoli ya watoto yamerudishwa Uchina kutokana na kuwa na sumu. Kuanzia wanyama Marekani mpaka watoto wamedhurika kwa sumu au kwa vifaa kutotengenezwa kwa kuangalia usalama wa watoto
CHA KUJIULIZA:
Hivi ni nani anafuatilia vifaa , vyakula hivi hatari, vikirudishwa Uchina vinapelekwa wapi?
Kiniogopeshacho ni kwamba inawezekana vifaa hivi na vyakula hivi , haviharibiwi.
Vinauzwa kwetu sisi Waafrika kwa bei ya cheeee.
Sina ushahidi na hili, lakini naamini kabisa hili jambo linatokea na lishatokea.
Si unakumbuka:
- Wamarekani wanamchezo wakutoa hata kwa msaada vile walivyostukia haviwafai kama vyakula au kwa nia nyingine zilizojificha zinufaizazo Marekani na sio Afrika . Unakumbuka hii?
- Meli iliyobeba uchafu wa sumu na kuupeleka Ivory Coast?
- Nestle´ na ajenda zao za kisiri Afrika?
- Mambo mengine mengi yaliyogeuza Afrika kuwa jalala.
Sasaaaa...
- Tuachie na Wachina wageuze Afrika jalala?
- Kama hatutaki kuachia, nani anafuatilia hizi mali za kichina ambazo zimejaa Afrika?
- AU ni mpaka tufe?
Afrika inabidi ijiadhari na mpenzi mpya huyu wa Kichina. Isije ikawa hata Uwanja mpya wa Tanzania ni moja ya jalala, maana nasikia ukijikwaa kwenye kiti kinaweza kung'oka.Ukifunga maji kwa nguvu unaweza ukaongoka na bomba zima la maji!
Tuwe macho na Afrika yetu hata kama katika swala hili haina bikira.
Duh!Naacha!
Baadaye basi!
Mpate Bilal akija na Soul Sista!
6 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
hapa umelonga ni kweli habari hizi zimeandikwa sana na vyombo vya habari vya magharibi.Lakini hapa kwetu kimya tu.
Na wamejaa tele ukubisha nenda sinza,kinondoni karibu nao watagombea ubalozi wa nyumba kumi tumekwisha na bidhaa hapo kariakoo ndio usiseme si kwamba wana maduka makubwa ya kutisha ni kama yale ya watani zangu na wamejaa haswa
Ni ukweli mtupu mzee kituturu,kwani swala la Africa kipekee TZ kuwa dampo ni makubaliano ya wakubwa kaka,wanavuta cha juu alafu sisi ndio tunaumia,tunabaki kunyoosheana vidole tu.lakini kaka ipo siku waTz watachoka na kufanya kitu kitakachoshangaza dunia.kaka kituturu kazi nzuri.
@Chediel na Honest:Kazi Kwelikweli
Katibu uemeeleza vizuri mkuu.
anani iwe nanyi.
samahani,amani iwe nanyi
@Rasta Luihamu:Asante!
Post a Comment