Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MANDELA na NYERERE watu NISHAI sana!

>> Saturday, September 01, 2007

Kuna watu wamebarikiwa kujua maswala na kujua jinsi ya kuyawakilisha maswala kwa jamii.
Kuna watu wanajua sana, lakini ujuaji wao ni vigumu kwa mtu mwingine kufaidika kutokana na wajuaji hawa kushindwa kujua jinsi ya ufikishaji wa wajuayo kwa wasiojua.

Kuna watu, maswala magumu kwako , ukikutana nao watakupa jinsi yakuyaangalia maswala hayo na kujistukia kuwa ugumu uliokua unauona unatokana na ile kona uliyotumia katika kuyapigia chabo hayo maswala.

Wakati nawafikiria viongozi wetu wa Afrika , huwa nastukia Mwalimu Nyerere na Mandela wanakakitu fulani kakujua jinsi ya kuwakilisha katika jamii wailengayo yale wayajuayo na hata wasiyoyajua.

Wanamchezo wa:

  • Kuyafanya mambo makubwa kuonekana madogo.
  • Mambo magumu kueleweka, kusikika au kuonekana rahisi sana.

Watu noma sana hawa!
AU?

Ningependa kuwa na kaujuzi kao, kakufikisha ujumbe kwa staili waitumiayo!
DUH!

Maswali:
  • Ushawahi kuwa na mwalimu ambaye darasa zima linajua anajua anachotakakufundisha, lakini kila mtu darasani hamuelewi na kuombea kipindi kiishe?
  • Ushawahi kuwa na mwalimu mjanja ambaye wote mnajua anakwepa maswali yenu kutokana na ukweli kila mtu anajua kuwa hajui , lakini mnafurahia uwepo wake darasani?
Duh!
Ngoja niache!
Wapate Freshlyground

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

luihamu 4:28 pm  

kuna wengine wakisoma unayoandika watasema umeishiwa na joya,lakini hoja yako imejificha ni kwale tu wenye upeo kama wa Nyerere na Mandela wataelewa unazungumzia nini.

Simon Kitururu 9:00 am  

@Rasta:Inawezekana ni ukweli nimeishiwa hoja!Si unajua kuishiwa hoja ni kwaisa kwa binadamu.Tatizo ni uwezo wakutumia busara na kukaakimya au kulazimisha hoja.Lakini yote ni ubinadamu.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP