Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

HIVI KWANINI TUNAONGEA NA MAREHEMU?

>> Saturday, September 29, 2007

Najiuliza tu!
Kuna mwenye uhakika kuwa, Marehemu alikuwa MTU Mzuri, ANATUSIKIA?

DUH!

Naacha!

R.I.P wote mliotangulia!

Swali:

  • Hivi kwanini tunataka MAREHEMU WALIKUWA WATU WAZURI, wapumzike mahali fulani wakati wengine waliotutoka tuna jua walikuwa wanafurahia kuchakalika sehemu sehemu kuliko kupumzika?
DUH!
Tulia na Awilo wakati ukifikiria kama nilichoandika ni sahihi au sio...
AU?



8 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

luihamu 2:55 pm  

KWELI MZEE KATIBU SIMON WAMETUTANGULIA NASI TUNAWAFUATA.

KIPINDI KILE BOB KAAGA DUNIA,PETER ALISEMA LET THE DEAD BURRY THEIR OWN DEATH.

Simon Kitururu 3:08 pm  

@Rasta Luihamu:
Lakini hii topiki ngumu kweli. Ukiiongelea sana watu hawatakuja kukuzika:-)

luihamu 3:39 pm  

HATA PALE ZAMANI HAWAKUZIKI BALI MAITI ZILITUPWA PORINI.

Simon Kitururu 5:05 pm  

@Rasta Luihamu:DUH!

Egidio Ndabagoye 8:33 pm  

Ebwana kweli,kuna sehemu niliwahi kuuliza kwanini marehemu aliliwe na kusemwa alazwa pema peponi wakati kila mtu mitaa ile alikuwa akisali usiku na mchana jamaa afe.

sikupata jibu zaidi ya kuangaliwa kwa jicho baya.

Simon Kitururu 10:40 pm  

@Egdio:
Kazi kwelikweli.

Egdio Umepote Mtoto wewe!

:-)
Napenda hiyo hapo juu ,kauli ya kiswahili maarufu kwa kutishiana.

Lakini , R.I.P waliotngulia.
Sijui wananisikia?
Nilishawahi kutishwa na Moses Kulola kipindi nilivyokuwa mlokole kuhusu jambo hili.
SASA NAHISI WOTE SISI TUNAANGALIWA KWA JICHO BAYA.

KKMie 12:00 am  

Si ndio hata mimi nashangaa! Mtu mlukuwa mnamchukia akifa mnaanza kuwaga misifa ambayo hana. Hivi ni uoga wa kufa au?

Egidio umenichekesha kwa maelezo yako, watu hulia kwa sababu tofauti:-

1-hawatamuona tena (mume, baba, mkware n.k.) inategemea na uhusiano ulionao na marehemu.

2-Jinsi gani ya kuendesha maisha ikiwa yeye ndio alikuwa kichwa....mama/baba na waliokuwa wakimtegemea.

3-Jinsi ya kukabiliana na wana ndugu kwenye swala la urithi (wakati mwingine unajuakabisa huna chako japo kuwa ulichangia ktk kuipata mali hiyo) basi kilio ndio huzidi.....mama/baba.

4-Uoga wa kurudisha namba(kufa) kwani akiondoka mmoja ujue namba yako imesogea hapo.....hasa kama mjamaa ameondoka kwa sababu za kingoma (UKIMWI).

5-Huruma, hofu, mashaka kwani hujui au huna uhakika anakwenda wapi? Na Ikiwa alikuwa muovu basi unasikia huruma kuwa anakwenda kuona cha mtemakuni.

Hey wandugu, Mungu anahuruma sasa kwanini tunaambiwa kuwa kunakuadhibiwa kutokana na makosa tuliyoyafanya Duniani?

Au the trick ni kuijua siku yako nakuomba msamaha b4 hand ei?

Ni matazamo msinitoe macho!

Kazi nzuri Si.

Simon Kitururu 2:39 pm  

@Dinah: Kweli kabisa usemayo.Lakini topiki ngumu hii kuiongelea.Tamaduni, mila, dini, halihalisi ya kifedha ya wahusika, mfumo wa serikali kujali watu wake, na mengine mengi yanachangia Mtu akuombeaye ufe, ukifa, anadai marehemu alikuwa mtu mzuri na hakosi kuja msibani kula ubwabwa. DUH!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP