Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KABLA HUJAMCHOKA KIPENZI!

>> Tuesday, September 04, 2007

Kipenzi,mpenzi.
Mtoto mzuri kweli!
Msichana analipa , si utani!

AU......

Kijana hendisamu , mwanadada hakawi kumuota zile ndoto nzuri nzuri zijazo hata akiwa macho!
Bonge la buzi.

Inawezekana hata jina hulijui , lakini umemtungia lako la kisiri!
DUH!
Penzi limenoga hata kama ni la alinacha!
Chochote afanyacho wakionea kwa upande mtamu.
Wale wakustuao kwamba nonihino anaupande mchungu usioujua , unawaona wachawi wanakuletea kiwingu.
Akijamba hunusi harufu mbaya!
Sana sana anakufanya ucheke kwani ni kichekesho tosha.
Anavyokoroma akilala, ni bomba la wimbo na kibembelezo masikioni mwako.

Siku zinaenda.............!

Hali halisi inaota makucha!
Kwa sababu hata uliponogewa ilikuwa ni hali halisi.
Kilicho cha maana na kisicho maana vinabadilishana viti.
Kifurahisho na kinachouzi vinagombania kiti kimoja.

  • Akikugusa kwa mapenzi , anakusumbua na kukumbusha uguswapo na nzi au buibui.
  • Akikoroma unahama chumba.

  • Ukimaliza kazi ofisini , unaanza kuwaza utafute kisingizio gani cha kuchelewa kurudi nyumbani.

Tatizo ...

Visingizio vipo.
Ukweli ni kwamba penzi limegeuka sura.
Ukweli ni kwamba humchukii mpenzi.
Kwasababu penzi likibadilika sura, bado ni penzi.

Ila...

Ni penzi jipya linalohitaji kuangaliwa kwa jicho jipya na kulipalilia kwa jembe tofauti.
Inawezekana inabidi mpaka ubadilishe hata mbolea, kwa penzi hili kustawi tena.
Kwani penzi hili ni rahisi kufichwa nyuma ya ....
  • Majukumu ya kulea watoto
  • Kazi nyingi ofisini
  • Matiti yamelala siku hizi
  • Umeota kitambi
  • Viagra hazipatikani kirahisi
  • au hata...... .
Lakini......
Kuishi na penzi jipya yawezekana.

Lakini......

Swali:

  • Unaruhusiwa kumchoka kipenzi na kutojisikia unafanyakosa?
  • Ushastukia kipenzi uliyemchoka waweza kumtamani ukimuona kadakwa na mtu mwingine?
DUH!
LAKINI......?

Siku njema!
Mpate Billy Ocean akikupa jinsi Ghafla alivyostukia kapenda!

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Serina 11:23 am  

Hata jivu halijapoa...Duh!

Simon Kitururu 5:27 pm  

@Serina:-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP