Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Ratiba ya SIKU YA KUFA!

>> Thursday, September 06, 2007

Baada ya taarifa za habari kujaa habari za kufariki kwa LUCIANO PAVAROTTI leo, na kumsikiliza Dr Remmy Ongala akiimba kuhusu siku ya kufa, nimeshindwa kujizuia kutafakari haka kamchezo ka-kufa na ratiba yake, ambako ni ka-lazima kwa binadamu wote kukacheza siku na mminyominyo ukifika.

Lakini.........

Ratiba, katika tamaduni nyingi ni kitu cha kawaida.
Tatizo ni kwamba , ratiba haina sura moja katika tamaduni tofauti.
Ratiba iaaminiwayo kuliko zote duniani, ni ile isiyo na vikolombwezo vingi ndani yake.
Ni ile isemayo kesho nitaamka, halafu nikichoka nitalala.
Hizi ratiba zenye sekunde, dakika ,saa , siku , mahala, zikiongezea na nitafanya nini katika muda huo, pamoja na kuwaletea mafanikio mengi wachache waliofanikiwa kwelikweli hapa duniani, kuna mambo mengine inacheza hola.

Lakini.....

  • Nisikufiche, ukiwa na ratiba na unauwezo wa kuifuata, kuna uwezekano ukafanikiwa sana.
  • Nasikitika , Tanzania , hatujafanikiwa kuweza kufuata ratiba kisawasawa.

DUH!

Siku zote ni tofauti.
Nikiwa na maana hakuna siku mbili zifananazo.
Hakuna mtu aliyeweza kuishi siku mbili akiwa ni binadamu yule yule.

Kila kiminyominyo, sekunde, dakika, siku....., binadamu anageuka, kuanzia chembechembe mwilini mpaka hamu yake na ujuzi wake wa utamu wa pipi.
Naamini unakumbuka, pipi uionjavyo mara ya kwanza ni tofauti na urudiapo kuimumunya baadaye.
(Kumbuka kiminyominyo au mminyominyo ni kipimo changu binafsi cha muda)

DUH!
Lakini....

Siku ya kufa , inaweza ikawa si leo, ingawa ni kama kesho!
Ratiba yake ni kama kesho tuifikiriavyo.

Swali:
Si unakumbuka hakuna siku mbili zifananazo?


DUH!

  • Unajua lakini, unaweza kupanga ufe saa na dakika ngapi? -nategemea ukifanya hivyo unajua utakuwa umejiua lakini.
  • Si unakumbuka mara nyingi wale wajilipuao kwa sababu ya kutetea dini, walioko kwenye fasheni siku hizi, huwa hawafanikiwi kujilipua katika dakika waliyopanga?

USISTUKE!
Kila siku , kuna watu magerezani na kwingineko waliopangiwa wafe dakika gani na ratiba inafuatwa kikamilifu.


Nawatakia wote waliofariki WAPUMZIKE MAHALI MEMA PEPONI!
Sijui lakini kama wote tuwaombeao wapumzike mahali mema peponi wataenda huko peponi.
Na kama wote wanaenda huko....... mmh!

DUH!
Kama unasoma hapa , inamaana wewe mzima, lakini haina maana mimi niliyeandika bado niko hai.

Ishi vyema, hatuna uhakika na ratiba!
SIKU NJEMA!
Nakuacha na marehemu aliyefariki jana, LUCIANO PAVAROTTI na marehemu aliye tutoka miezi kadhaa iliyopita. JAMES BROWN:

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Anonymous 11:59 am  

asante KM kwa kutuletea muziki hii. Safi sana.

Simon Kitururu 12:25 pm  

@Kifimbocheza:Poa Mkuu!Tuko pamoja!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP