Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Binadamu Kwa Mashindano!DUH!

>> Tuesday, September 11, 2007

DUH!
Nilipotea kidogo.
Nimerudi sasa!:-)

Ngoja niende kwenye kilicho mawazoni....

Tabia ya kutafuta nani zaidi , imezoeleka sana katika shughuli mbalimbali za binadamu.
Na kwa kweli huwa wanampata nani zaidi kwa kutumia vipimo kemukemu ambavyo mara nyingine ni vigumu kuelewa vipimo vyenyewe mara nyingi.


Swali:
Hivi ni nani Mzuri kuliko wote?
Nani anaakili kuliko wote?
DUH!
NANI ZAIDI?
Si wote ni binadamu?


  • Nashindwa kuelewa kwanini kuna mashindano ya wasanii.
  • Nashindwa kuelewa Kwanini kuna mashindano ya Uzuri!
  • Nashindwa ku....
Nirahisi kuuona ushindani kwenye sanaa, michezo ,siasa ,lakini uko kila kona.
Nirahisi kusikia watu wakijiuliza kuwa hivi:
  • Hi Hukwe Zawose au Moris Nyunyusa
  • Ni Mr Nice au Dudubaya ni zaidi?
  • Bob Marley au Peter Tosh ni zaidi?
  • Michael Jackson au Prince?
  • Miles Davis Au Louis Armstrong?
  • Ngwasuma au...............
  • Ni Richa Adhia au Hoyce Temu
Naamini kila msanii ni bomba.
Naamini kila mtu anapenda kitu fulani, ambacho masikioni au machoni mwake kinapendeza.
Naamini kitu kizuri kwangu sio lazima ni kizuri kwako.
Lakini!
Duh!


Tukienda kwenye michezo, inasemekana ushindani ni afya!
Lakini kuna michezo kama formula 1 ambayo pia nashindwa kuamini kuwa ,ingawa dereva ndio anasifika kuliko wote, kama ni kweli anastahili kuwa na sifa zote zile.


Kushindana labda ni ubinadamu.
Kwa sababu ninauona sana ubinadamu kwenye mashindano ya kisiasa.
Mwenye nguvu na hela mara nyingi ndio huibuka mshindi.

Nakutakia kila la heri katika ushindani!

Nawaza tu!
Usitishike!

Pata picha fulani ambazo hazija poa.
Lakini tulia na wadau wa senegali waliotuburudisha....

(Mtimkubwa unasalimiwa na Maissa na timu nzima ya Gallaxy)

PICHA ZA KIKAO CHA WADAU WA TIMU YA BONGO FC HELSINKI
Powered by www.myfabrik.com


Lakini ngojea tupate dondoo ya kitu fulani kiaandaliwacho...

AU hukustukia eeh!
Endelea kupata dondoo..


Tuendelee na picha....
Dj EZZA na Magonella
Powered by www.myfabrik.com


Niliowakata ni kwasababu tu sikuomba kuwapiga picha.Natumaini hakuna noma.Sijatoa sura nzima:-)
Powered by www.myfabrik.com

Picha mchanganyiko
Powered by www.myfabrik.com


Tuko pamoja!
Siku njema!
Tulia na Common

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Anonymous 7:08 pm  

Custo,

Asante kwa picha na salamu toka jamaa wote hususani wazee wa Galaxy.

Jioni hii nimetoka klabu moja katikati ya jiji la Gothenburgh inaitwa Nefertiti kuangalia mambo. Klabu kiboko kwa kila kitu; location, interior design, size, sound system na mengineyo. Yakitimia tutawasiliana ili tupeane mikakati.

Tafadhali naomba uwafikishie jamaa wote salamu nyingi sana. Nakutakia kila la kheri na mafanikio.

Ni miye nduguyo,

F MtiMkubwa Tungaraza.

Simon Kitururu 3:43 am  

@Mtimkubwa!Asante kwa salamu.Salamu zako zitafika.Tuko pamoja!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP