Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Jamaa wanachuki na mimi ,NDIO MAANA NIMEPANDISHWA CHEO KAZINI!

>> Friday, September 14, 2007

  • Shikamoo bosi!Ulaji unanizidi?

Wanaojiita wajanja fulani, hudai kuwa cheo kizuri ni kile kinachokupa ulaji wa haraka.
Unaweza ukakuta jamaa kachukia, anakuna kichwa, kisa amepandishwa cheo .
Katika mazingira ya kawaida unaweza kushanga ni kwanini jamaa hafurahii kupandishwa cheo!
Lakini , utapewa jibu hata pale kwa fundi viatu kwa kusikia porojo zisemazo ; tutaona sasa atamaliziaje nyumba ya kimada wake sasa ,wakati kaondolewa kwenye ulaji.

Naogopa ofisi zisizoeleweka na zisizo na taratibu ziwezeshazo kufuatilia nini kinaendelea.
Kwa bahati mbaya hizi ofisi ni nyingi na nyingine zinajulikana kwa jina Ikulu..
Katika ofisi ambayo haina mbele wala nyuma zaidi ya viini macho na majina ya vyeo vya wajipumzishao ofisini, unaweza kukuta ni dereva au mesenja wa bosi ndio mlaji na aendeshaye mambo kuliko yule Kikwete wa ofisi.

Mara nyingi tunamzungumzia bosi mambo yakienda vizuri au vibaya.
Lakini katika hizi ofisi
  • unaweza kukuta mesenja ndio tajiri, halafu haachi kazi ingawa ana hoteli kadhaa na teksi kibao pale kona.
  • Unaweza kukuta ni aitwaye dereva wa bosi, mwenye nguvu ofisini, anaamua misafara ya bosi na bosi anaitikia kasuku kasingiziwa.

Swali:
Hivi katika serikali ya Marekanni ni George Bush mwenye nguvu?

Nachojaribu kusema ni:
WAKATI unafikiria jinsi ya kumnyima bosi ulaji, kumbuka unaweza ukawa umelenga pembeni ya goli.Inawezekana hata bosi mwenyewe hajastukia kuwa hausiboi wake nyumbani ndio mjanja,kuna kaasali kanakosababisha anajilamba na kukubali mshahara mdogo.

Na pia tusisahau kutafakari haka kakitu ujanja, kwa maana janja nyingine mimi na wewe tunazifagilia lakini manufaa yake ni msamiati mgumu.
DUH!

Kuna kawimbo ka Jimmy Cliff kako mawazoni......
Kapate basi:

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP