Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

WAKATI , naikumbuka SikuKUU Ya Milleniamu ya Ethiopia....

>> Friday, September 28, 2007

Samahani !
Kabla sijaanza........,
.........angalia picha ya MTU aliyesababisha unaamini, tarehe uliyozaliwa ndiyo yenyewe.

Naamini unajua jina lake laki -PAPA alilojipa.
Si alivyozaliwa alikuwa anaitwa Ugo Boncompagni.
DUH!
Mcheki basi!























Swali:
  • Umezaliwa siku gani vile?

  • Hivi Ukiwa umezaliwa tarehe 29 mwezi wa pili, aka Februari 29. Bethidei zako unazifanyaje mwaka usiofikia februari, 29?
Nikiongelea tarehe ,
siongelei Maulidi wala Krismasi ,aliyoibadili au kugundua
MJANJA.

DUH!

Dondoo:

Naamini unajua kulikuwa na kalenda nyingine enzi za wanzabanga!

AU?



Binadamu ana mambo ya ajabu,
anayofikiri kuwa anayajua.

  • Kama wewe Binadamu, usibishe!

DUH!

  • Bisha!
Kwa sababu Simon, anasema, yaliyoko mawazoni mwake, ambayo ni wewe unauhakikanayo, kwasababu, shehe na mchungaji wako, bila kumsahau , baba, mama , mwalimu , au yule umuaminiyo, ambao wamejua maswala kutoka kwa .............amesema ingawa huko kwa... huna uhakika ni ukweli.


DUH!

Swali:
  • Waliokufundisha wayajuayo, wamejifunza kutoka wapi? (Au wameshushiwa ujumbe pale kilimani ambako hakuna aliye shuhudia?)

DUH!

Wakati nchi nyingi ziliacha kutumia Julian Kalenda baada ya makubaliano ya wajanja wakiongozwa na Papa Gregory , akisaidiwa na aliyeanzisha utundu wa kubadilisha , aitwaye Aloysius Lilius, kalenda ikabadilika kutoka ya ki- ROMA kwenda...

DUH!

Nisikufiche !

Narudia Swali:
  • Una miaka ufikiriayo unayo?
AU niulize .....
  • Hivi unafikiri unamiaka mingapi?
  • Hivi unafikiri utafanya nini ,ukijua uchovu wa kalenda ikufanyayo uamini leo ni ijumaa, na ......kuwa Waithiopia , Waroma, na Sisi, tumfuataye Papa Gregori na...... kuwa tunacheza pata po.... .......?
DUH!

Si endelezi!
Nimeacha!
AU?

Samahani kidogo naingia kwenye Ubudhisti....

Naamini wewe muislamu usiyefuata kalenda ya kiislamu, nakufuata ya Papa Gregori, isemayo leo ni tarehe 28, na wewe ufuataye kalenda ya Papa gegori ambayo ingekurusha miaka saba ndani ya siku moja, Papa na kikundi chake walivyoamua kubadili siku kutoka za kiJULIAN kwenda Kigregory,kuwa leo ni miaka saba zaidi, na wewe ufuatayo kalenda nyingine ambayo kama Muislamu umefunga, kama mimi , unaweza ukawa unafuturu sasa hivi, kwa mambo ambayo kama wewe ni Mkristo unaweza kuamini baraka fulani za utamu sijapewa na......

(Dondoo:

Umependa sentensi yangu ndefu hapo juu,isiyo nampangilio , bila kukwazwa?)

Samahani nagusia kwenye mwanamme na mwanamke...
DUH!

  • Uliyekuwa unaamini mvulana akidinda na binti akapata mimba kuwa walifanya utundu tarehe fulani....Hiviiiii....MNAFUATA KALENDA GANI na YA MJANJA GANI?
Ngoja tupate kwasababu gani wanaume hawatosheki na uhusiano na KIPENYO, mpaka wapate VIPENYO



SAMAHANI WANADADA!
DINAH!
Nipe mambo!
AU?

NIPENI Wanadada upande WENU uelezao KWANINI HAMUTUWEZI, TUKIWA WENGI TUKIwaSHEA?

SWALI :
HIVI KUnaukweli WANAWAKE, hamtujumlishi?


UKiRISTO
HAUJANIPA JIBU!




DUH!


Samahani nakuondoa katika maswala hapo juu, na....

Au Unayakumbuka?

Jisahaulishe basi...!

Swali
  • Hivi hizi ndombolo za solo aka ngwasuma, tuzipendazo Tanzania, tunaelewa wanasema nini? Hasa wakiimba vizuri kwa lugha za kingwasuma?
Nisikufiche ,!
Nanihii na...zinachezeka na najua tunaimbiwa kwa kiswahili nyimbo kedekede!

AU?

Turudi kwenye Kalenda...

  • Katika kubadili kutoka Juliani mpaka Gregori kalenda, ilichukua dakika moja ambayo inasababisha, Ethiopia iwe miaka saba nyuma leo hii kutoka katika miaka ambayo, Tanzania inafuata.
Swali:
Hivi Watanzania, wabudhisti, mbona hawastukii kila tarehe muhimu zisizo za kidini, hazifuati tarehe za kiislamu?

Kwasababu ,
naamini, wanadini, hasa Wakristo na waislamu, wana nyege za kufuatilia mambo fulani ambayo ukigusa kuongelea kinamna naongelea, lazima uungue.

AU?

Samahani lakini!

Kwenu wote Wanadini, hasa wakristo ,kwa kuwazingua !
MsiniSOKOINE BUREeee !
Kisa niko mawazoni,
wala hata gari la ubunge na ... sijapata.

DUH!

Naacha!

Nitaanzisha kalenda yangu karibuni.

Atakaye kuifuata anyoshe kidole juu!
DUH!

Ushawahi kufikiria utajisikiaje mara tu ukigundua miaka yako imeongezeka kwa miaka saba ndani ya siku moja, kama leo, kwasababu nimeamua, kutokana na ushauri wa muangalia anga?

DUH!

Usitishike!

Mpate Busta Rhymes atulize...
Samahani lakini!
Haongei lugha nzuri.

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP