Wadau EEH! ASANTENI! TUKO PAMOJA!
>> Wednesday, September 05, 2007
Kuna kitu rahisi sana kusahau!
Nacho nikuwashukuru washikaji wanaotupa kampani kila siku katika shida na raha.
Mimi kama Mdau ambaye kwa miaka zaidi ya Kumi na tatu nimekuwa naishi mbali na nyumbani,marafiki na wadau mbalimbali ninaokutana nao au kujuana nao ni muhimu sana kwangu, na wamekuwa msaada mkubwa kwangu kiakili na kimaisha.
Mnikosoavyo na mnifundishavyo ni muhimu sana kwangu.
Bila nyinyi nafikiri ingekuwa vigumu kuweza kuwa Simon mmjuaye.Na nafikiri ningekuwa mpweke sana katika maisha haya ambayo unapoishi, hata jirani humjui zaidi ya kupungiana, na hilo ni kwa bahati bahati hasa katika maisha haya tuishiyo yaendayo kwa spidi kali.
Nashukuru sana kwa yote!Ningependa kutaja majina lakini itashindikana kutokana na wingi wa washikaji zangu ambao wote ni muhimu.
ASANTENI SANA!
NA SAMAHANI KWA WOTE NILIOWAKWAZA NA KUWAKOSEA!
Unajua tena miye ni binadamu!
Ngojaniseme....
Usistuke hakuna sauti, nakuzingua tu mdau!
Lakini....
Ngoja niweke baadhi ya picha zangu na wadau niliokuwa nao ndani ya siku hizi chache zilizopita.
(WADAU WENGINE POPOTE DUNIANI NISAMEHENI! MNAWEZA KWENDA MOJA KWA MOJA KWENYE VIDEO YA X-plastaz , chini kabisa ya post hii.)
DUH!
Kabla ya picha wadau tuliokuwa pamoja mnakumbuka hii?:-)
Clemoo uliniua mbavu.
Mnakumbuka hii pia......?
Picha za baadhi ya washikaji wangu siku chache zilizopita na mimi...
Kwa mara nyingine:
ASANTENI WADAU WOTE!
Siku njema!
Na tulieni na X Plastaz
7 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
A Day in the Life of Simon. Safi sana.
@Da Chemi:Ingekuwa mali kweli kama kila siku zingekuwa zinaenda murwaa!Maana siku nyingine ukiamka tu unaanza na kujikwaa wakati unatoka kitandani.
Washikaji ni muhimu sana ukiwa mitaa ya mbali na nyumbani.Nami nawashukuru washikaji wa mitaa hiyo kwa kutokukuangusha.
@Egdio: Ukiwa pekee yako hukawii kurukwa na akili.
yule mdada wakisonjo anavyopiga shot duuh kama msoviet kazi kweli ulaya maanke hii action ingekua kule mogadishu ni murder case
@Aliko:Si Utani!
Safi kwa kifupi nimeikubali. nami nicheki ktk http://artsfede.blogspot.com/
Post a Comment