Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

IMANI YAKO ITAKUPONYA!UKIWA VUGUVUGU HUTA URITHI UFALME WA...

>> Friday, August 31, 2007

Kuna dini fulani zilinifundisha kitu muhimu sana kwenye maisha.
Ziliniambia kuwa karibu kila kitu kinahitaji sana na kinauhusiano sana na imani yako katika kitu hicho.

  • Ukiamini umekula chakula kichafu hotelini baada ya kugundua msalani kuchafu na ni pembeni ya jiko walilopikia na waliko wafadhili wale nzi wahitajio chakula kama wewe, unaweza kuharisha wakati huna vijidudu vilivyokududua.

Nilijifunza kuwa ukiamini kuwa kuna......... na ndio jibu , basi ni mpaka uamini kikwelikweli kuwa kalekadude ni ........ ndio katakuwa jibu.

Niliambiwa...
  • Imani yako ndio itakuponya.
Inamaana, ukiwa na imani haba, hata ukaokoka vipi, lakini kama hujaamini kisawasawa, jehanamu ilo karibu na ndio chobisi yako ukianza kinamna.
  • Nikaambiwa kuwa ni lazima uwepo ndani ya hekalu, au ,ujitoe kabisa chumbani, kwa sababu , mguu nnje-ndani = na uko nje.
DUH!
Nisikufiche!
Haka kakitu kako mawazoni sasa hivi.
Halafu nakaamini kikwelikweli......
  • Naamini ukitaka kale kakitu na kama unaamini kabisa nilazima ukapate kale ka....
  • Naamini kale kakitu utakapata hata kwa njia uifikiriayo sasa hivi, na sio ile ya mkato aliyokutonya mshikaji kuwa........
DUH!
Kumbe mshikaji ni wewe!
Nong'oneza tu njia ya mkato kama ni halali!

  1. Lakini , njia ndefu inafaraja zake.Inakusababishia kujua na kukasikilizia kale ka-utamu kunoga kinamna fulani.

Utakua unajua kwanini na kwa njia gani ambayo umekatolea jasho kukapata kale kakitu bila mjomba kukasaidia au yule mwingine kukupunguzia utandu kwa kudai kuwa; Simon bila mimi asinge......

Usiniulize lakini kama kale kakitu nimekapata tayari au bado!:-)
DUhh!
Najua kuna watu wana haraka sana hata katika..........!

DUH!
Sasaaa.........

Si imani yako itakuokoa?
Si imani yako itakuponza?
Swali :
Imani yako inaku.................?


Pata....

8 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Suojeluskunta suojaksi Suomenmaan 3:30 pm  
This comment has been removed by a blog administrator.
eddiie 6:32 pm  

Always a pleasure dropping here....until i learn Swa...i think its a good walking ground..

Thanks for dropping by...Eeeh!! you had gone through a lot...

Simon Kitururu 6:40 pm  

@Eddie:Nice to know that my crib doesn't bore U!I think swahili aint that difficult if U put Ur mind into it!
Find a Tanzanian girlfriend, it might help!:-)

Anonymous 8:42 pm  

kale kakitu sitauliza kama umeshakapata...au kama upo mguu ndani-nje...lakini maswali haya nusunusu...

Anonymous 8:49 pm  

Asante pia kwa muziki...I'm doing fine:)

Simon Kitururu 9:05 pm  

@Serina:Hivi ni kweli haya maswali ni.....?:-)

chemshabongo 12:09 pm  

kaka mjibu serina maswali yake usimpe nusunusu.
tupo pamoja

Simon Kitururu 4:48 pm  

@Chaemshabongo:Mbona nimemjibu?Sijamalizia sentensi kuachia kisehemu cha mtu kutumia imajinesheni!Si unajuatena alinacha, ndoto na .....

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP