Wachina wana akili!Waafrika je?
>> Thursday, August 30, 2007
Katika kipindi hiki ambacho China inazidi kuwa na nguvu!
Katika kipindi hiki ambacho wachina wameingia kisawasawa Afrika mpaka kwenye biashara za umachinga!
Katika kipindi hiki ambacho unasikia mpaka ni jinsi gani kila kona ya dunia inavyokiri kuwa Wachina wana akili....!
Ni rahisi kusahau kuwa cha zaidi wakifanyacho ni kugundua kasehemu waaminiko kana utamu na kukalamba kisawasawa.
Swali:
- Si ni ukweli pamoja na watu kuzidiana akili(kama hicho kitu kipo) ,bado wengi tuwaitao majiniasi, siri yao kubwa ni ujuzi wao wakugundua pointi yenye utamu na kugundua jinsi ya kuilamba kwa nguvu zote?
- Lakini si ni ukweli si kazi ngumu kugundua pointi yenye utamu karibu kwa mtu yeyote?
- Tatizo si ni jinsi tu ya kugundua jinsi ya kuilamba nukta yenye utamu?
Niligongana na watu waliokuwa wanashabikia kuwa Wachina wanaakili sana.
Sipingi!
Nachojiuliza ...
Swali:
Kwani nani hana akili?
Ndio , ukifuatilia historia utagundua kuwa ni Wachina waligundua karatasi, poda za risasi, hata.....
Ndio , sasa hivi uchumi wao unakua kwa kasi ya ajabu. Inasemekana moja ya kazi ya wachumi wao kuu ni kupunguza kasi ya ukuaji wa uchumi ili kuweza kuudhibiti ukuaji.Kitu ambacho sisi katika nchi za Afrika tunajaribu kukuza uchumi wetu na hata kama haukui kisawasawa viongozi wetu hawakawii kutuambia uchumi unapaa.
Lakini katika historia pia utakuta jamii ya kichina , kizungu , na kiafrika vyote vilifanya makosa na mazuri yake.
Wazungu walistukia utamu uko wapi na wakaulamba kwa nguvu zote!
Wachina walishaustukia zamani lakini wakachemsha mpaka Wazungu wakawazidi na kuwatawala.
Swali:
- Kama Mchina aligundua bunduki, unafikiri ilikuwaje Mzungu akaja kuwatawala kwa kutumia bunduki aliyogundua Mchina?
- Si sisi waafrika wengi tulishindwa kwa Wazungu kutokana na wao kusaidiwa na kuwa na bunduki?
- Ikiwa Mchina aligundua bunduki na kuja kutawaliwa na mtu aliyejifunza kwa Mchina bunduki ni nini......
- Ikiwa Mchina aligundua karatasi.....na mpaka sasa anajifunza mambo mengi tu mengine watu wengine walioandika kwenye karatasi......
Naamini kuwa agunduaye si lazima afaidike zaidi ya aliyekopi jinsi ya kulamba.
Tatizo ni kwamba kila nukta B yenye utamu si lazima ilambwe kama nukta A.
AU?
Chakujiuliza:
- Inakuwaje mchina anaweza kutoka kwao na kuwa machinga Afrika na kufanya umachinga kama wamachinga tulivyowazoea?
- Je,kastukia kuna kautamu na kastukia kuwa wakalambavyo waafrika ni sawa ila yeye anaongeza nguvu tu?
- Kwani sisi Waafrika tunakosea wapi?
Katika kuongea na kujadiliana na watu duniani , ni rahisi kukutana na Waafrika wenye uwezo mkubwa wakufikiri na kufanya mambo na wako kila kona duniani wakionyesha maringo yao dingiridingiri mpaka chini.
Sasaaa........
Hivi pamoja na yote haya.......
Pamoja na ukweli tunajua utamu uko wapi......
- Je, ni jinsi ya kulamba bado hatujajua , au ni spidi ya kulamba tuitumiayo ni ndogo kiasi cha kufanya tujikute tunaambulia kijisehemu kidogo tu cha pipi?
Duh!
Basi bwana ngojea niache!
SIKU Njema!
Namuacha SUGAR DADDY akiendeleza kufagilia SOCA
0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment