Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

WEWE ni MLEVI eeh?

>> Saturday, August 18, 2007

Hadithi ! Hadithi!

H
apo zamani za kale alitokea kiumbe fulani , kipindi hicho alikuwa hana jina. Huyo kiumbe akagundua utamu, uchungu na katabia kabaya.............

Tabia yoyote ni tabia mbaya kama haioani na kipimo jamii ikichukuliacho kama ni sahihi.
Lakini ........

Ngoja niseme..........

Katika akili ya binadamu ya kuunganisha maneno na tabia , imefanikiwa kuonisha maswala mengi tu yasiyo husiana na kitu chenyewe, ila yakatafutiwa sababu za kibinadamu kuoanisha hayo maneno na jambo hilo, kitendo hiko na hata hisia hizo.

Swali:
Unafikiri utamu neno na utamu uhisio ,vina uhusiano?
Wewe una uhusiano na jina lako?

Duh!

Turudi kwenye hoja......

Pombe si chai!
Pombe nishai!
Lakini pombe yako yaweza kuwa ni kahawa!

DUH!
Tatizo la kilevi ni pale lilivyoweza kujiweka katika sura ya aina yoyote.

Kilevi chako waweza kuwa unakiita jina tofauti Lakini!
Usistuke!

Kwa mfano kilevi huweza kuwa:

  • Mke wako.- ambaye bila yeye akili yako haitulii
  • Kazi yako.- bila hiyo , kila kukicha unakumbuka kujishusha kibinafsi pale uonapo wenzako wanaenda kazini.
  • Mpira wa miguu.-ukufanyao usipate muda wakufuatilia kama watoto wako walimaliza kazi za shule walizo ambiwa wazifanye nyumbani.-ikufanyao ughairi kuangalia taarifa ya habari na kumalizia ile shughuli.
  • Chakula.- ambacho kikinukia tu hukawii kushindwa kuwaza jambo jingine lisilohusiana na mlo.
Swali:
Ushawahi kuwa na kile kitabia cha kulamba sukari watu wasipo kuangalia?

Ndio sipingi kuwa matatizo ya kilevi yanazidiana kutokana na aina ya kilevi na pia yule aathiriwacho na kilevi chenyewe.

Si siri , tatizo la ulevi, ni kwasababu ulevi umegeuka kuwa ulevi.Unalewesha!

Lakini kumbuka.....
  • Wengi hulewa kwa sababu zihusianazo na furaha na kuishi
  • Wengi hulewa kwa sababu zihusianazo na matatizo na maisha
Utamu wa kaulevi, kila mtu ana kipimo chake.
Usishangae kuona :
Wengi wakipigania kautamu ka ulevi au kutoelewana tu kutokana na kaulevi hako!

LAKINI WENGI WATAPIGANA NA KUTOELEWANA KUTOKANA NA UKWELI KUWA WAME LEWA.

ULEVI Katika MIZANI ya SIMON leo HII:
  1. DINI
  2. Sehemu za siri
  3. Pombe
  4. Chakula
  5. Nguvu(Ubwana mkubwa wa kijinga)
  6. Na......
  7. Nk
Duh!
Burudika na Miriam Makeba

6 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Anonymous 4:17 pm  

kuna vilevi vingine afadhali kushinda vungine...au sivyo?

Simon Kitururu 9:55 am  

@Serina:Si utani!:-)

Aliko 1:34 pm  

duuuh

luihamu 3:34 pm  

Kwa mtazamo wangu,vilevi vinakufanya udhania umefika kumbe haujafika,kwanini katika mikutano mikubwa huwa wanaruhusu watu kutumia vilevi baada ya mkutano au vikao.Kama hivi vilevi ni vizuri kwanini waalikwa husubiri bibi na bwana harusi wakifika ndio waanze kutumia vilevi.Linganisha na ukumbi wa wa disco,ukiingia unaanza kutumia,hakuna taratibu za kunywa.
Kilevi aina ya pombe kinapotosha ukweli wa halihalisili ya maisha yako,unacheka siku moja lakini unahuzunika miaka nenda rudi.Mimi naita BABYLOAN SOUP.

bINADAMU YEYOTE HAWEZI KUMEDITATE KAMA AMETUMIA POMBE KWANINI?
KWANINI VIJANA WANGE WANATUMIA POMBE ILI WAFURAHISHE TENDO LA NDOA?Hapa mzee katibu utasikia vijana wakisema,huyu ngoja nitamnywea bia hizi tano then atakoma.

Mimi naona njia moja ya kilevi ni kukamata jembe,rato,sururu,mbegu,mbolea na n.k.

Simon Kitururu 5:09 pm  

@Aliko: :-)
@Rasta:Inategemea binadamu unaye muongelea anataka ninni. Si binadamu wote wanataka ukweli au wana taka kufikiria ,kumediteti ua ku... kama binadamu wengine watakavyo.
Binadamu wengine pamoja na yote watakayo , wako poa tu na kufanya kinyume na binadamu mwingine apendavyo. Sehemu nilipo kuna binadamu wanafanya umalaya kwa hobi!Ingawa sehemu nyingine watu wanatetea kuwa hali ya maisha ndio inafanya watu nni malaya. Unakumbuka kama wengine watakavyo kuishi kuna watu wako tayari kujiua dakika hii. Kuna....

luihamu 6:15 pm  

Sawa kabisa Katibu.
Naamini kabisa si rahisi kubadilisha maisha ya binadamu hata umpe nini.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP