UBINADAMU WAKO SHILINGI NGAPI?
>> Friday, August 17, 2007
Kabla sijasema, ngojea DATAZ na Joan wakukumbushe maswala ya MUME wa MTU!
Binadamu huthamanisha maisha ya binadamu bila hata kufikiria wanafanya kamchezo hako.
Ukiongelea ughali wa maisha mara nyingi watu huupima kwa kipimo cha pesa , mali na....
Uthamani wa maisha ya mtu, wengine huupima kutokana na ukaribu wao na huyo mtu.
KWA Mfano , uthamani wa mtu utokanao na:
- Undugu wako naye
- Huyo mtu akuathirivyo kifikira, kimaisha...
- Umpendavyo au kumchukia huyo mtu
- Umuoneavyo wivu
- Maamuzi na tabia zake zikuathirivyo kibinafsi , kimaisha, kiimani na....nk
Uzuri na ubaya wa maisha tafsiri zake ni binafsi. Maisha ya mtu mwingine waweza kuyatolea macho kwa kufikiri ni baabu kubwa kumbe hakuna kitu. Na kunayule unayempita chobisi hata bila kumuangalia mara mbili kutokana na jicho lako lilivyojaa kasumba ya nini baabu kubwa, na likakuambia yeye nishai , kumbe ndio mwenye siri ya nini muhimu katika maisha na ndio alaye maisha.
Jicho la mtu mwingine limtazamapo mtu mwingine na kufikia hitimisho kuwa jamaa maisha yake :
- Mabaya
- Mazuri
- Anakula raha
- kaharibikiwa
- anajiua
- anaaafya
- ana....
DUH!
Ngojea tupewe Vidonge na Malika (Asha Abdow Suleiman)
SWALI:
- Ukiona maiti za watu usio wajua au unyanyasaji uendeleao duniani;kina kuuma zaidi wahusika wakifanana nawe(kirangi,kidini,maadili nk)au kwa kuwa ni binadamu?
- Ukishabikia michezo , hasa timu usizozijua , unavutiwa na mchezo wachezao katika kuamua unashangilia timu gani, au kwa sababu kunajamaa unafanana nao?
- Nimeanza kufikiria ni mizani gani jamaa waliofanya biashara za utumwa waliyotumia kujua bei ya binadamu(mtumwa)!
- Hivi bei ya kunanihii inapatikanaje pale kona ukitaka kunanihii kwa kulipia?
- Bei ya nazi je?
Duh!
Ijumaa njema!
Nakuacha na kakumbukumbu kafupi kaenzi hizooo!Donna Summer..
0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment