Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MWANAMKE HUWEZA KUKOJOA KASIMAMA!

>> Thursday, August 23, 2007

Wanaume huweza kukojoa wamechuchumaa.
Tatizo ni binadamu waliofanya liwe tatizo hili swala la staili ya kukojoa!
Duh!
Inasemekana wanawake wakikojoa wamesimama ni rahisi kujikojolea.

Lakini.....

  • Ukifuatilia swala , utagundua kuwa staili ya kukojoa si muhimu kama uwezo mzima wa kukojoa
Ukishindwa kukojoa ni kasheshe.
Na ni jamii tu imeamua kuwa kujikojolea ni nishai!
Nahisi kama mikojo ingekuwa inanukia pafyumu, marashi yanukiayo kama harufu ya mikojo tuijuayo hivi sasa, yangekuwa ndio ujanja kununua.

Sasaa....moja ya nachomaanisha katika insha hii ya mikojo.....

Enzi zile za mababu, uwe mwanamume usiye na misuli fulani yakuwindia,kulima, ku... staili yako ya kuleta chakula nyumbani isingefanana na ya mwenye misuli na kufua kama simba.

Karne hii , huwezi ukamdharau asiye na misuli , kwani anaweza kuwa anafikisha msosi nyumbani kuliko weye mwenye misuli kama simba.
Mwanamke na mwanamume, hawatofautiani sana katika kufikisha matakwa ya kimaisha chobisi.
Mwanamume na Mwanamke wote hukojoa , hata kama ni kwa staili tofauti.

Wewe kama unachuchumaa, unakaa, au unasimama katika kukojoa haina maaana sana.
Cha muhimu unakojoa!
  • Fanya kwa staili yako yoyote , ili mradi unapata upatacho kihalali.
AU?
Namuachia Jack Radics

6 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Evarist Chahali 8:09 pm  

Nimekusoma Mzee.....

eddiie 8:10 pm  

I really cannot read Swa...but easy man..i will always pass here..I love passing by and wont stop...Am taking lessons in Swa..and soon we shall be pamoja ebana...

Anonymous 12:11 am  

Kaka SK, mie nishawai kuona mwanamke anaye kojoa kama amesimama wima wima! DUH! Ningeweza kukueleza kinaga ubaga jinsi alivyoweza kufanya hivi lakini naogopa wasomaji wako wakanikemea...!LOL

Howz my swahili by the way?

Simon Kitururu 4:34 am  

@EvaristNimekuona.Usinitenge lakini.:-)
@Eddie: I will keep trying on writing in English on my other blog, but I want and hope U keep visiting my Swahili blog.Tuko pamoja!:-)
@XS: Si utupe tu stori!Ur Swahili is good. Lete kinaga ubaga basi!Wasomaji wangu wataelewa!
AU?

Bob Sankofa 11:26 am  

Kaka blogu imezidi kuwa nzuri. Umepata wapi hii templete au umeunda mwenyewe?

Pamoja kaka!

Simon Kitururu 9:01 pm  

@Bob:Nimetengenezewa hii na mshikaji.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP