Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Zawadi ni kitu kizuri! Unapenda Embe Ng'ong'o EEH?

>> Wednesday, August 15, 2007

Kabla sijasema !Unamkumbuka Ndala Kasheba?

Unatakiwa kutochagua zawadi upewayo. Tatizo la zawadi ni kwamba , tunajitahidi kuioanisha na kitu kizuri.
Kitu kizuri kina tatizo, Kwa sababu , kitu kizuri kwako kinaweza kuwa kina nijazia tu , sio kabati tu , bali hata chini ya kitanda.
Nisikufiche, huwa na nunua maua kwa wapendao maua.
Zawadi ni kitu cha ajabu sana. Ukisikitikia zawadi, ukiwania zawadi, au ukichagua zawadi , hiyo si zawadi.Zawadi kwa Athumani na kwa Zubeda zina tabia tofauti.Lakini...

Swali:
Hivi zawadi ni nini? Si ni embe ng'ong'o tu?Si lile shati, chupi, kondomu na.....?
Au vitu vya bure ukipewa ndio zawadi?

DUH !
Kuna wadau zangu hupenda viatu!
(Ngojea Kelly aseme ingawa naomba kama wewe mdogo usimsikilize)....


Akili ya binadamu nishai! Zawadi anazijali kutokana na kakitu ambako binadamu mwingine anaweza kukajua ingawa binadamu wengi uchagua kutojua hako ka kitu ambako wengi wao hujiumiza kichwa kutokana na ukweli hawajui Zawadi ni nini.
Swali:
Zawadi kwako ni nini?

Nashukuru kupata zawadi fulani kutoka kwa watu walio jua zawadi kwangu ni nini.
Asante kwa Kitabu. Unajijua uliye nizawadia hicho kitu!
Asante kwa Ukarabati wa Blogu hii!Unajijua uliye nizawadia hicho kitu!
Samahani kwa wote niliyo wa zawadia kitu walicho fikiria kumpa yule jamaa chobisi kutokana na kutopata nguvu ya kuniambia ile haikuwa Zawadi!
Duh!
Kawimbo fulani ka zamani ka Wayne Wonder na Buju Banton Kako akilini. Kasikilize basi...

Ngoja niache!
Baadhi ya picha za Jana kwa KANYE WEST

Powered by www.myfabrik.com

Duh!
Hebu subiri kidogo.....

Duh!Kumbe walikuwa wanakataza kurekodi na hata kupiga picha eeh!
Ngojea basi niziache picha nyingine za siku ya Kanye.....Ben , Aliko na ....eeh, Asanteni!
Powered by www.myfabrik.com

Nakuacha na Kanye ...

Siku njema!

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP