Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MAANDAZI YAPO, UNAHAMU YA KUONJA VITUMBUA?

>> Thursday, August 23, 2007

Kila kitu hukinaisha!
Ukitamanicho jua kunamtu kimemkinai!
Si unajua kinaa cha:

  • Kula vitumbua kila siku!
  • Kwenda kanisani kila mara!
  • Ugali kwa maharage kila siku!
  • Kula kuku kila siku!
  • Kwenda chooni kila siku!
  • Kunywa tule tubia kila siku!
  • Kupigia chabo kale kakitu !
  • Ku...........nk.
Swali:
Si unajua kwenda haja, pamoja na kuwa ni lazima kama umekula, kuna kastarehe kake?

K
wa binadamu ni rahisi kuona kautamu ni kakijani zaidi katika kisamvu kilichopo sufuria jingine. Maswala ya kutaka kujua , kuelewa uzuri wa vyetu kwa kuona au kuonja vya wenzetu, pamoja na kashule tupatako, yanatuponza mara nyingi.

Lakini....

  • Wewe ungejuaje kuwa Zubeda au Abdallah wako ni mzuri , ikiwa hakuna Anna au Wilson wa kufananisha kakitu?

  • Ungejuaje utamu wa chai yenye sukari kama hakuna chai isiyo na sukari?
Mimi sipendi sana maandazi kama vitumbua .

Sasaaaa.....
UKWELI, na si ni kaBUSARA fulani, kama sio ujanja, kuvumilia na maandazi hata kama vitumbua hupatikana?

AU wewe unataka vyote?
Ukipata vyote ni nishai?

DUH!
Siku njema!


Tulia na Tshala Mwana Akikupa kibao MBOMBO

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP