MSAFIRI KAFIRI!Haja Ikibana, Breki ya Choo Hupungua Nguvu Ufikapo Chooni!
>> Tuesday, August 14, 2007
Kabla sijasema ngojea ST Germain waturudishe kwenye mudi.......na Sure Thing.
Kuna mambo mengi ukiyakaribia kakitu fulani hupungua.
DONDOO:
- Enzi za kukariri kabla ya mtihani , unaweza kujikuta fomula fulani unazotaka kuziingiza akilini baada ya mlango wa chumba cha mtihani kufunguliwa , huwa akili inajaribu kuzikataa wakati wewe unajaribu kuzing'ang'aniza zikae akilini.
- Ushawahi kubanwa na haja zile mbili maarufu(Kubwa na ndogo)kisawasawa , halafu ukaanza kustukia breki ya kuzibana inaanza kupungua nguvu mara tu ufikapo msalani nakuanza kuangaika na zipu?
Ngoja nikupe vistori VINNE, basi vya safari zangu nisizozisahau......
Kila safari inasura yake. Na mara nyingi ni kawaida kutokwenda utarajiavyo. Lakini safari ni shule fulani, kwani hukawii kujifunza mawili matatu kuhusu wewe mwenyewe bila kusahau kujifunza pia kutoka katika mazingira unayokutananayo.
- Sisahau safari moja ya kwanza iliyoganda akilini, iliyonifunza matumizi ya choo na unishai wa kulakula.Nilikuwa nasafiri kutoka Mbeya kwenda Kilimanjaro na famili.Kipindi hiki nilikuwa na miaka mitano. Kinamna nilifanikiwa kushika mfuko uliokuwa na kilo kadhaa za karanga.Basi kwa kutumia ujanja nikafanikiwa kuzila zile karanga sana tu.Matatizo ya kula kila mtu anayajua, ni lazima choo ndio hitimisho.Enzi hizo za mabasi ya KAMATA , inabidi umsitue kondakta kuhusu maswala ya kuchimba mzizi. Mimi na utoto wangu enzi hizo nilichanganyikiwa. Kwa kuogopa kustukiwa nimekula asilimia kubwa za karanga za wote, nikawanaogopa kusema kuwa tumbo lishachafuka.Kilicho niokoa nisiachie kinyesi chepesi ndani ya nyeti, ni jinsi nilivyodhoofika na sura ilivyobadilika kwa kujitahidi kuzuia kinyesi chepesi kwa nguvu zote.Shangazi yangu aliyekaa karibu yangu alipostukia maswala nakuomba basi lisimamishwe nikachimbe mzizi , nilikuwa katika hali ya hatari. Nilipofika nje ya basi wala sikuhangaika kwenda mbali kwani breki zilianza kukataa. Kitendo hiki kilinisababishia kutupa chupi porini na kusafiri safari nzima bila chupi na kutaniwa kwa miaka kadhaa na ndugu na jamaa. Kitu hiki kikanifundisha matumizi ya choo kabla ya safari na pia umuhimu wa kuwa na kiasi katika vile vitu uvipendavyo.Unajua tena mimi pamoja na kuwa mvivu wa kula , karanga na vinywaji fulani huwa vinapanda.DUH!
- Safari ya pili nisiyo isahau, ni ile iliyotokea mwaka 1980 wakati famili nzima tunahama Mbeya kwenda Songea. Hii safari ndio ilinifunza ni nini kinaweza kutokea katika barabara . Barabara yakwenda Songea kipindi hicho ilikuwa mbaya sana. Nafikiri katika Landrover niliyokuwepo, ni mimi tu na dereva walikuwa hawatapiki. Safari ilijaa harufu ya petroli na matapishi kitu ambacho mpaka leo hakinitoki akilini.Ukiachana na watu kutapika mpaka matapishi hayatoki, barabara ilikuwa inapita katika sehemu inayo itwa Lukumburu, ambako ni kwenye udongo wa mfinyanzi. Katika milima hiyo kila bonde unaloangalia kulikuwa na mabaki ya magari. Kutokana na kusafiri wakati wa mvua ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza kuona magari yamefunga breki lakini yanakwenda kutokana na udongo kuteleza. Basi kwa mara ya kwanza nikaingizwa katika matembezi ya hiari katika matope na msitu usemekanao una Simba.Watu waliamua kumuacha dereva aendeshe mwenyewe na kutungoja baada ya mlima kuliko kuwemo ndani ya gari lisilo funga breki kutokana na utelezi.Safari hii ilinifunza mengi, mojawapo ilikuwa; mtu huhofia sana akionacho kuliko asicho kiona katika mazingira fulani.Tulikubali kutembea ingawa kunauwezekano kuwa tutembeapo tutaliwa na Simba kuliko kuwepo ndani ya gari ambalo ninaonyesha dalili zote za kutuua. Kabla ya hapo nilikuwa nafikiri mtu huogopa tu kile asichokiona kama giza. Si unakumbuka zile stori za kutisha, za majini nk. ambazo nilikuwa napenda kuzisikiliza wakubwa wakiongea halafu naogopa kuzima taa wakati wa kulala?DUH!Kakitu haka kamenikumbusha jinsi gani baadhi ya binadamu tunamuogopa yule tu anayeonekana ana UKIMWI.Akiwa ana UKIMWI lakini hauonyeshi ,basi twende kazini. AU?
- Baada ya kufika Songea , kila mtu akaapa kutotumia magari kwenda sehemu nyingine. Kipindi hiko uliweza kutumia likizo yako yote njiani kwa kutumia mabasi au magari kutokana na ubovu wa barabara za kwenda Songea.Njia iliyojitokeza ikawa ni ndege. Watu walikuwa wanasafiri na ndege za jeshi za mizigo kama kawaida. Kitu ambacho siku hizi ukisisitiziwa ufunge mkanda kwenye ndege kama ulipitia kusafiri na ndege za mizigo zisizo na viti unakuwa na jeuri kidogo.Ndege nyingine za abiria za Air Tanzania zilikuwa ni zile ndogo ndogo za Focker (watu 42 kama nakumbuka vizuri). Kipindi hiki nakikumbuka kutokana na mvuto uliokuwa unatokea ukiwa katika ruti ya kwenda Dar , wakati wa kukatiza maeneo ya Mto Rufiji.Hapa ndege ilikuwa inarudishwa chini kwa sekunde fulani unajisikia unaelea.Halafu unarudishwa tena kitini ndege ikienda juu.Kitu nisicho kisahau ni jinsi katika safari yangu ya kwanza na hizi ndege za aina ya Foka zenye injini mbili, ilipotokea kuwa katika kasheshe za mvutano injini moja ikazima. Tulisafiri chini chini mpaka Dar-es Salaam Airpoti kwa injini moja.Yale maswla yakuona mawingu juu yalisahaulika. Nachokumbuka ni kuwa kila mmoja alikuwa anaomba sala fula .Ila kulikuwa na Mhindi mmoja mweusi ambaye ndiye alikuwa mhindi wa kwanza mweusi kumuona ambaye yeye safari nzima alikuwa anapiga picha wakati wengine wanalia na kutubu dhambi zao. Kitu kikubwa nilichojifunza kuhusu mimi katika safari hii ni , nauwezo wa kutulia katika mazingira ambayo kila mtu amepaniki.
- Safari ya nne ambayo niliifurahia ilikuwa ya kwenda Nairobi. Niliifanya na Kaka yangu Davie Kitururu. Tuliamua kutembea kwa miguu kwenda kenya. Safari hii ilianza kama utani tulipokuwa Arusha na kutaka kuchukua taxi mpaka Nairobi.Si unayakumbuka yale mataxi ya kushea? Duh!Ngoja niache basi......!
Bado sija kaa sawa kutoka na maswala ya safari....Lakini ngojea nikuache na baadhi ya picha za safarini.
Kabla ya hapo ngojea tudake baadhi ya safari za mzigo....
Kamzigo kupakiwa kwenye kadege fulani....
Kamzigo kaingiapo chobisi fulani.....
Powered by www.myfabrik.com
Ombaomba walikuwepo hata sehemu usizotarajia...
Powered by www.myfabrik.com
Msafiri kafiri
Powered by www.myfabrik.com
UL(l)EVI
Powered by www.myfabrik.com
Baadhi ya Marafiki njiani!Kuna wngine nimestukia hampendi kupigwa picha:-)
Powered by www.myfabrik.com
Safarini baadhi ya picha zaidi..
Duh!
Ngojea niache....!
Bado sijarudi kisawasawa katika kublogu.
Swali:
Ushastukia kila siku stendi/Stesheni /kituoni kuna watu wanasubiri usafiri?
Dondoo:
Maisha ni safari!Safari usizofanya kwa kutumia baiskeli, miguuu na ....unazifanya kimawazo!
SAFARI NJEMA!
Lakini ...TUKO PAMOJA!
Namuacha COCOA TEA na DENNIS BROWN wakikumbusha maswala ..... Getting Myself Together..
6 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Duh!
Kuna kastori kamoja siasoma hapo juu:)
Simon, Simon, Simon...
Umenikumbusha mbali mzee, mambo ya kuchimba dawa...
Ukisafiri na basi, konda akisimamisha mchuma kila mtu anafuta mti au kichaka chake cha kujificha...wengine wakizidiwa hata peupe pweee wanaachia...
@Serina:......:-)
@Metty Mambo yakuchimba dawa kiboko:-)
makini kaka!!!!
na umerudi kwafujo balaa, punguza kasi tupate muda wakupitia kila post, na wale ombaomba pale juu nawo wapo kwa bwana joj kichaka au?
@Chemshabongo:Nitapunguza kasi!Lakini unajua tena kuna siku ni rahisi kuandika kuliko nyingine.Ombaomba kwa joji wapo.lakini hapo juu ilikuwa si kwa mista Kichaka:-)
Post a Comment