Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Ukiwauliza Watoto Wakikua Wangependa Kufanya nini!

>> Wednesday, August 08, 2007

Kabla sijasema ngojea nimuache Chris Isaak aseme baadhi ya jambo ambalo baadhi yetu huombea tukikua tufanye...lakini....


Ukimuuliza mtoto akikua angependa afanye nini, unaweza kupata majibu kama ningependa kuwa:

  • Dereva wa magari!(Eti nasikia nchi nyingine huwa wanachagua kuwa madereva wa magari ya Zimamoto.Duh!Naombea magari haya yawe mengi na kwetu bongo)
  • Polisi
  • Daktari
  • Mwalimu
  • Muuza duka
  • Na.............
Lakini baada ya kuingia katika mfumo na kuanza kunyoshwa na hali halisi ya maisha kuna mambo mengi ambayo unajikuta yanakubadilisha muelekeo wa kutoka kutaka kuwa Polisi na kujikuta mlinzi nyumbani kwa mtu au kujikuta......
Badala ya kuwa muuza duka , unastukia ni muuziwa gongo
Badala ya.....

Cha kawaida ukishakuwa mkubwa ni kujaribu kufikiria kamaungelijua ungefanya hivi na vile ulipokuwa mdogo ili maswala yako yawepoa zaidi sasa.

Maswala mengi kama watoto tuyafikiriayo kuwa tungependa kuyafanya tukikua, yanaongozwa na kutojua hali halisi ya shughuli hizo ukubwani. Na maswala mengi ambayo tunafikiria sasa hivi kuwa kama muda ungerudishwa nyuma tungefanya vingine, hutokana na ukweli kuwa hata ukweli halisi wa hali halisi tuliyonayo hivi sasa , hatuujui kwa asilimia mia.Kwa hiyo siwezi kushangaa kuwa , hata ukirudisha muda nyuma na kuanza upya kuelekea upande ambao sasa hivi unafikiri ndio bora, unaweza kufika huko uelekeako na kufikia hatima ileile uliyoifikia sasa hivi kuwa; ukipewa nafasi nyingine ya kurudisha muda nyuma ungefanya mambo vingine mwaka uleeeeee.........

Dondoo:
Ukweli ni kwamba , tulipo sasa hivi ndio hali halisi ya maswala. Mengine ni alinacha.Piga ua lakini hakuna ujanja zaidi ya kudhibiti hali halisi ituzungukayo sasa hivi.
Duh!

Ngojea nimuachie Sorab Wadia Akiigiza kama Hussein Al Mansour aelezee atakavyo kuwa kama Osama Bin Laden

Sasaaa....
Da! Ngoja niache...
Siku njema!
Tulia basi na Safari Sound Band wakikupa Chakacha

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP