Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Udongo Uukanyagao Yawezekana ni Mabaki ya Maiti Fulani!

>> Tuesday, August 07, 2007

Kabla sijasema!
Mpate John Lee Hooker akisikitikia mji wake ulipokumbwa na mafuriko.

Kuna watu wanadai kuwa dalili za siku ya mwisho ni haya majanga kama mafuriko, tetemeko la ardhi, volcano kulipuka nk.

Lakini ukifuatilia historia ya dunia utakuta kuwa milima na mabonde pamoja na maafa kibao ni moja yayaliofanya dunia iwe kama ilivyo.

Sehemu kubwa ya tabia ya binadamu imejengwa kutokana na binadamu kushuhudia watu wakifa njaa, kuumwa na nyoka,kupigana vita nk.

Lakini cha ajabu ni kwamba hitoria mpaka leo imeshindwa kuwa ni kitu cha uhakika kumfanya binadamu asirudie kosa.

  • Sehemu nyingi zikumbwazo na mafuriko na kuua miaka iliyopita usishangae zikaua tena siku nyingine kutokana na wakazi kutokuhama au kuyaendeleza maskani ili yasidhuru.
Sehemu kibao zinazokumbwa na majanga ya aina fulani ni mara chache watu kujifunza na kuepusha majanga ya baadaye.

Sisi binadamu ni kiboko kwa kusahau kirahisi. Nahisi maswala ya Oldoinyo Lengai kutokana na kwamba mlima haukulipuka mambo yashasahaulika.

Swali:
Ukisikia mtu kafa na UKIMWI unatishika siku ngapi?

Sisi binadamu huwa pia na kamchezo kakuuana halafu tunadai tunaogopa maiti. Kwa jinsi tunavyokufa na tulivyokufa nahisi karibu udongo mwingi tuukanyagao ni kaburi la kitu fulani. Maiti ya panya ,ndedere mwanakaka au mwanadada inaweza kuwa ni moja ya mbolea irutubishayo kaudongo fulani usikokaogopa wakati una ogopa kupita makaburini na unaogopa maiti.

Duh!
Ngoja niache !
Mpate tena John Lee Hooker aponyeshe na wimbo The Healer akiwa na Santana


Mwandani, unakumbuka tulikuwa tunamsikiliza huyu John pamoja?

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

KakaTrio 4:59 pm  

Dah simon imenichukua muda mrefu kupata sehemu ya kuandika comments kwa maana ilikuw ainasema "KOMENTIA" wakati macho yangu nimeyatrain kutafuta comments!

Anyways nimeona unapost picha nyingi katika ujumbe mmoja au posting moja nikaona nishee kitu ambaco nimekiona kwnye bulogu zingine cha namna ya kushea picha nyingi kwenye post moja hii kitu inaitwa filmloop na web yao ni http://filmloop.myfabrik.com/ kusema kwlei nimeipenda sana. Hebu angalia hapa huyu jamaa wa Zenj kaitumia hio technologia nafikiri itakusaidia sana na wewe hapa kwenye bulogu yako na itatufanya sisi wageni wako kufuraia zaidi picha ambazo huenda hunaga nafasi ya kutuletea.

Ahsanta

Simon Kitururu 5:08 pm  

@Maricha:Duh!Naona blogger yangu inaongea Kifini. Nitaifanyia kazi.
Asante kwa ushauri wakutumia Film Loop. Nitaijaribu hivi karibuni.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP