Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KATIKA KUPIGANIA UHURU WA KUJAMBA!

>> Sunday, August 19, 2007

Kujamba hadharani nishai!
Nakubali , kijambo kinanuka.

Swali:
Si ni kila mtu hujamba ?
Lakini kwanini tunaona aibu kujamba sehemu fulani?

Turudi kwenye hoja......
Nia ya kuwa na uhuru ni kutaka kuwa na uhuru.
Nia ya kuwa na uhuru wa kufanya tu, tuyapendayo , ndio moja ya njia itufanyayo kukosa uhuru.

JAMII NI JELA.
Inatujengea misingi ya uhuru ambayo inatufunga.
Inatufanya...

  • Lile panki ulilokata nishai!
  • Ule msuko uliosuka nishai!
  • Zile rasta ulizonazo nishai!
  • Zile nguo ulizovaa nishai!
  • Zile tamaa zako nishai!
  • Lile kabila nishai!
  • Yale matako nishai!
  • Yule hausigeli/hausiboi umpendaye nishai!
  • Ile rangi nishai!
  • Na.....Nishai!

DUH!

Unajua.......

  • Tokea tupate uhuru kama nchi, tumekosa uhuru wa kutokuoanishwa na nchi fulani!
  • Tokea uoe/uolewe, umekosa uhuru wa kula sambusa fulani ambazo huzidi kujitokeza baada tu ya ulipochukua kitumbua!
  • Tokea ujulikane kama mwenye busara, mkubwa,... umekosa uhuru wa kufanya ujinga!

Swali:

Ujinga kama we ni binadamu, ni nini?

DUH!

Tulia na STEVIE WONDER!


7 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

luihamu 3:44 pm  

Mzee Katibu,kujamba ni afya lakini nashangaa.

Simon Kitururu 5:00 pm  

@Rasta Luiham:Nahisi navyoongelea kujamba unachukulia kuwa niliongelea kujamba kama kujamba kujulikanavyo. Nilivyoandika namaanisha kitu kingine ingawa nafikiri wengi wamesikia harufu kama wewe kwa sababu ni rahisi mawazo kuchukulia hivyo.Ukifikiria zaidi utannielewa.

luihamu 6:10 pm  

Katibu ngoja nisome tena.
hii blogu yako nani katengeneza au ni wewe mwenyewe?

Rundugai 7:27 am  

Kweli uko mawazoni haya Kujamba gani huko.Kama si huku kwa kawaida

Simon Kitururu 10:11 am  

@ Chediel:DUH!
@Luhiamu :Hii blogu nimetengenezewa na mshikaji kishikaji.Unaionaje?

Anonymous 4:24 pm  

Blogu safi kabisa! DUH
Nipe basi digits za huyo 'mshikaji kishikaji' nimpe kazi! LOL

Simon Kitururu 6:19 pm  

@Inexes:Mshikaji anakusikiliza!:-)
Asante lakini kwa kuifagilia Blogu!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP