Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Hivi ni nani masikini kuliko wote Duniani?

>> Wednesday, August 08, 2007


Powered by www.myfabrik.com
Wakati waoshavinywa wakilumbana kati ya Bill Gates na Carlos Slim nani anapesa zaidi.....kuna sura mamilioni hazinakitu

DUH!
Swali:
Hivi Utajiri ni nini?
Umaskini je?
Hivi ukiwa huna kitu maana yake wewe maskini?

Nilijikuka katikati ya ubishani wa kuwa nani nitajiri kuliko wote duniani. Katika gumzo hilo walio wengi wanauhakika kuwa tajiri kuliko wote ni Carlos Slim Mexicano/Mlebanoni, bepari mmoja. Wengine wakawa bado wanadai kuwa ni Bill Gates.
Mimi bado niko mawazoni , nikiwaza;

  • Hivi kwanini wenye pesa ambazo hata matumizi ya pesa hizo hawana wanakuwa ndio waonekanao kuwa wanaumuhimu kuliko wengine katika jamii yetu?
  • Hivi ushawahi kujiuliza kwanini kazi fulani za muhimu, mishahara yake ni mibovu ukilinganisha na umuhimu wake katika jamii yetu? Hivi hata malipo mengine kama heshima kwa wafanyao kazi fulani muhimu ni jambo kubwa sana katika jicho la jamii hii tuishio?
Duh!
Hivi manesi/ walimu na akina David Beckamu/Tiger Woods ni nani muhimu zaidi katika jamii?
Usitake kufananisha mishahara yao lakini, kwa sababu ..............

Umaskini nishai!Ila umaskini si kukosa pesa tu, tukumbuke hilo. Kwa sababu pesa ni kamchezo fulani binadamu amejitungia na masharti yake yamekaa kibinadamu. Leo unazo ukiwa nazo nyingi, kesho hata ukiwa nazo nyingi, hazina mpango.

Swali:
Unakumbuka Zimbabwe na pesa zao?

Naacha hii ....!
Cheki tu madansa hawa Lacey and Danny wakikuchezea Samba katika kulainisha siku na kukuapa nguvu ya kuendeleza libeneke....DUh!sina uhakika lakini kama utapata nguvu:-(


Photos kutoka:
Queenzy
India Ink
Wikipedia:
Bill Gates
Carlos Slim

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP