Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Si Umestukia Mungu Haongei na Miungu Haiongei Moja kwa Moja na Mtu wa Kawaida?

>> Wednesday, August 29, 2007

Dini karibu zote zimehitaji utashi wa mtu fulani na akili za mtu fulani kuwa kiunganishi cha watu na Mungu au Miungu yao.

Lakini....

Swali:
Imekuwaje Mungu na hii Miungu haijifungui kwa binadamu wote kirahisi mpaka watokee binadamu wengine kuwaelezea wengine maswala muhimu ya wokovu wa mioyo yao?

Lakini.....

  • Umestukia kuwa waletao dini chobisi na watambulikao kuwa ndio wanajua maswala haya, ndio wale pia wavaao vizuri, nyumba nzuri , wanakula vizuri kuliko wale watu wawalishao neno la Mungu au sentensi za Miungu?
Nakubali kuwa si miaka mingi sana iliyopita ilikuwa ni kawaida kutojua kusoma na kuandika. Ni kikundi kidogo cha waliojua kusoma na kuandika kilichopata maswala kutoka katika vitabu fulani na kutuletea katika jamii. Kikundi hiki kidogo kilitafsiri Mungu anasema nini, kutokana na ugumu wa kumuelewa Mungu na ugumu wa kuielewa hii Miungu.

Lakini...
Kumbuka kuna kikundi pia ambacho hakikuhitaji kujua kusoma wala kuandika kukupatia maswala ya Miungu au Mungu na kukusababisha ulete wale mbuzi na kuku kwa ajili ya kustawisha mihogo yako pale shambani, au hata kustawisha imani yako.
DUH!
Swali:
Inakuaje wengine wanajua mpaka siri za Mwenyezi wakati wengine hatujui?

Kweli labda kila mtu anakipaji chake cha kuelewa mambo fulani. Na Labda Mungu na Miungu pia huongea na watu fulani moja kwa moja kutokana na tofauti zao.
Swali:
Si unakumbuka kusali na kuswali eeh?
Hivi si tunaamini ni Mungu na Miungu hii ndio iliyotuumba wote ?

Nisikutishe lakini !
Labda wale wakutafsiriao kuhusu imani yako wanajua kuliko wewe kutokana na uzoefu na kuijua dini kuliko wewe.Labda wao wanaimani zaidi yako hivyo wanapata maono zaidi yako wewe na mimi.

DONDOO:
ushawahi kustukia kuwa asemekanaye ni wakwanza kustukia Mungu au Miungu , mara nyingi hutumia maneno kama....
  • Alioteshwa ndoto...
  • Alishukiwa....
  • Alitokewa na malaika
  • Ali....

Sijui kwanini lakini wanashukiwa watu mmoja mmoja katika dunia ya mamilioni.
DUH!
Ngoja niache haya maswala ya Mungu na Miungu!
Labda ni Mungu na hii miungu ndio ijuayo zaidi haya maswala!
Nakuachia wewe mwenyewe na ...
  • Shehe wako
  • Padre wako
  • Mchungaji wako
  • Bi kidude wako
  • Mzee Mghosi wako ................mwenyewe, haya maswala !

Turudi katika maswala ya dunia.......
Soca!
Ngojea nimuachie Machel Montano aseme..

Si unamkumbua Machel Montano alivyokuwa mtoto? Hebu furahi naye ndani ya SOCA


3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

eddiie 4:35 pm  

Ni me rudi tena..aki sii click that much...but am learnin...

Good to always drop in hear..Uko poa?..i hope so..aaaah!!

Simon Kitururu 6:12 pm  

@Eddiie:Niko poa!Karibu tena!

Anonymous 8:05 am  

Please call me soon ok? I'd like to hear from you...

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP