Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Baada ya Kugundua Wakubwa Hutukana!

>> Wednesday, August 29, 2007

Utoto nishai!
Inahitajika ukue ilikugundua baadhi ya maswala ambayo wakubwa wanafanya na wakubwa husemekana kuwa ndio wanayajua.

Nakumbuka nilivyokuwa mtoto nilizani kuwa baba yangu ananguvu kuliko watu wengine wote.Niliamini kabisa anaweza kupiga watu wengine wote.Navyosimuliwa ni kwamba, nilipohudhuria msiba fulani wakati mdogo , nikiwa na familia, nilichoelewa ilikuwa ni kwamba baba kawapiga wote waliokuwa wanalia pale msibani.

Elezo hilo ni rahisi kulizungumzia kwa kastori kama hapo juu, lakini ukilichunguza....

  • Utagundua , mimi kama mtoto, nilikuwa tayari nimeshaelewa kuwa moja ya kazi ya baba ni kuchapa. Nafikiri pia hili lilitokana na kuamini kupiga ilikuwa sio kazi ya mama kwa kuwa mama yangu ni mpole asiyependelea hata kufinya ukiharibu mambo.Kwa busara yangu ya kitoto nishastukia kazi mojawapo ya baba.
  • Utagundua kuwa kizazi kikubwa tuishicho, kimekuwa katika mazingira ambayo mara nyingi kipigo na sababu ya kipigo havikuwa rahisi kuhusishwa.Tulikuwa tukijua tu nani anayetoa kipigo hata kama kosa si wakati wote tulilijua, na labda tungelijua kitu fulani ni kosa tusingefanya hicho kitu hata bila kuchapwa.
Swali:
Unafikiriaje maswala ya kuchapwa?
Mbona tumekuwa vizuri tu baada ya kuchapwa sana , au umedhurika?
Lakini hawa watoto wakuao sasa bila kuchapwa je?

Ukubwa nishai!
Unaamka tu siku moja unastukia eti wewe mkubwa.
Kama Mtized unastukia unaanza kupewashikamoo, mara jina linaanza kubadilika, baadhi ya watu wanaanza kukuita Mzee!

DUH!

Cha ajabu, si kweli wote waitwao mzee au wale wakubwa kwa umri na kwa... maana yake wamestukia ukubwa wao.

Na kwa bahati mbaya.....
  • Ukubwa haumaanishi busara.
  • Busara kwa mmoja inaweza ikawa ujinga kwa mwingine.
  • Busara mara nyingine inatokana na ufahamu wa mambo.Hii inamaana kama hujui unaweza ukatumia busara kufanya ujinga.(si unakumbuka maswala ya wenye busara kugawa almasi kwa malipo ya pipi?)

Lakini.....
Kuna ambao wamekulia mazingira ambayo ilikuwa kawaida kusikia wakubwa wakiongea kila aina la jambo.Kuna waliotukanwa tokea utotoni. Na tupo ambao tulifikiri wakubwa wanajua kila jambo kiasi kwamba waliyosema ndio ilikuwa ukweli.

DUH !
Sentensi mbili:

  • Zamani ilikuwa kidogo maswala mengine yamefichika. Wakubwa waliweza kusikiliza mpaka nyimbo ambazo kwa enzi hizo ilikuwa ni matusi , bila ya mtoto kustukia wimbo unasema nini. Kulikuwa hakuna mitandao vyanzo vya habari vingi ambavyo utaibia na kustukia mtoto anazaliwaje. Unakua ukiamini kunandege kamleta au mama kaenda kumnunua kutoka duka fulani yule mtoto.
  • Siku hizi bado kuna mambo mengi yamefichika kwa wengi. Wakubwa wanaweza kusikiliza mpaka nyimbo ambazo kwa enzi hizi ni matusi, bila ya mtoto kustukia wimbo unasema nini. Kuna mitandao na vyanzo vingi vya habari ambavyo utaibia na kutostukia mtoto anazaliwaje. Unakua ukiamini kunandege kamleta au mama kaenda kumnunua kutoka duka fulani yule mtoto.
Lakini labda niseme....
Kwa watu fulani ambao ni wengi kabisa, na ambao wanaweza kustukia na kugeuza mambo...

Ni vigumu kuwaficha mambo.
Mambo yako siku hizi nje nje sana.
Matusi yako wazi mno.
Cha ajabu ni kwamba tutukanwao hatuchukii tutukanwavyo matusi ya kikweli.

Mfano wa matusi yatuudhio ni :
  • Meno kama ngiri wewe!
Mfano wa matusi tutukanwayo kila siku watu wazima na akili zetu ni kama:
  • Mimi mwanasiasa nawaletea ari mpya na nguvu mpya!
  • Uchumi wa nchi unapaa!Wakati tunaona wananchi wakizama.
  • Salamu ; Habari za nyumbani! Jibu:Nzuri tu !Wakati unajua mambo nishai!
Swali:
Hivi mtu akiwa anakufanya wewe mjinga kila siku, hilo si tusi?

W
akubwa hutukana na wadogo huiga hata kabla ya kujua mkubwa alilosema ni tusi.
Nasikitika kuwa sina uhakika kuwa matusi waliyokuwa wanatukana wakubwa zamani kwa mafumbo ni bora kuliko siku hizi tutukanwapo hadharani hata bila aibu.
Swali:
Tunavyokua na kujua pia wakubwa katika angazao huongea matusi , inamaana nasi tukikua tutukane?
SIKU NJEMA!
Mpate Lord Kitchener akikupa kitu DR KITCH



2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Anonymous 2:48 pm  

Learnt a new word today - nishai! Any relation to nishawai? (i have)

Simon Kitururu 6:15 pm  

@Excess!:sidhani kama kunarelation.Hatajiui asili ya neno hili ni nini.Huwa linatumika kumaanisha :mambo si mazuri, mambo yanatia aibu nk.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP