Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Wadogo/Wanyonge wakipata nguvu!

>> Friday, August 17, 2007


Kabla sijasema, Musical Youth wako mawazoni...Wasikilize kidogo...

Wadogo wengi hukosa sauti kutokana na udogo wao.
Wanyonge wengi hukosa sauti kutokana na unyonge wao.

Lakini.......
Duh!
Simon akiwa mdogo wa miaka mitano hapo chini....

Powered by www.myfabrik.com


Tatizo ni moja tu!
  • Wadogo walionyimwa sauti na kujiamini haina maana wakikua watakuwa na sauti na watajiamini.
  • Mnyonge si kweli ukimpa muda atafuta unyonge.
Saikoloji ya anyimwaye sauti au mnyonge inategemea na mtu mwenyewe. Kuna mnyonge anakubali unyonge kutokana na unyonge ulivyomuathiri .Kuna aliyekosa sauti na ataendelea kutotumia sauti yake kutokana na kutojiamini hata apatapo nafasi ya kutumia sauti.Ingawa kuna mnyonge ambaye kutokana na kunyanyasika , moja ya maana ya kuishi kwake, itakuwa ni kuweza kujitoa katika unyonge na kupaza sauti wote wasikie.

Samahani kidogo....
Kasikilize kawimbo kengine kahawa watoto(Musical Youth) enzi hizo zetu......

Kinachofariji ni :
  • Mdogo ananafasi kubwa ya kuwa na sauti na mamlaka akuapo. Ukiwa unamnyanyasa kwa udogo wake, jiandae kwa kukabiliana naye akuzidipo ukubwa.
  • Mnyonge kama Mjusi, ukimsakama , hugeuka nyoka.
LEO katika MIZANI YA SIMON:
  • Mtanzania kama mnyonge, bado ni mjusi.Sasa hivi anazidi kusakamwa na hali mbaya ya maisha , uongozi mbovu nk..Kumbuka sisemi viongozi wote wa TZ ni wabovu. Naamini kisa cha mjusi kuchelewa kugeuka nyoka Tanzania ni kutokana pia na kuwepo Viongozi ambao wanajitahidi kivyao na kwa uwezo wao kikwelikweli.Bado sijui ni lini huyu mjusi atageuka nyoka Tanzania!Wewe unahisi lini kama mambo hayabadiliki?
  • Wadogo wakikua , watakuwa na sauti, ingawa sijui watasema nini. Sina imani na wajengwavyo kifikira, kikuona mbele, hasa katika maswala ya kuona majibu katika matatizo.
DONDOO:
Mwenye sauti si lazima ajue kuimba!
Mwenye sauti si lazima anachakusema!
Lakini mwenye sauti anaweza kukohoa!

Swali:
Weye mwenye sauti na unacho chakusema ,unasema nini?

DUH!
Ngojea nikupige dozi ya mwisho ya Musical Youth baada ya kukua, wakiimba ule wimbo wao uliowapatia umaarufu wakiwa wadogo.

Je unafikiri walipokua wakubwa , wakiwa na sauti kubwa wame.....

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Kibunango 10:57 pm  

Kama utahitaji kusikiliza vipande vya Music Youth basi nitembelee, siku ambayo utapita Tampere

Simon Kitururu 12:49 pm  

@Che!Kibunango eeh! Mimi na sababu kadhaa za kupitia chobisi yako ,ila kama Musical Yuti watakuwepo ndani ya nyumba, hiyo bonasi!:-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP