Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kama UMEKINAI kufanya kwa siri, FUMANIWA YAISHE ili YAANZE!

>> Friday, November 14, 2008

Kama bado ulikuwa hujajiandaa watu wengine wajue ufanyacho, unaweza kufumaniwa kwa kitu ambacho UNGEWEZA tu kuweka wazi mwenyewe WATU WAJUE kuwa kilema chako WEWE DUME ZIMA , ni matiti hayana CHUCHU.

Lakini....
....Labda kila siku unaanza hata kama unaanzia ulipoachia jana.
Labda unaendeleza kwa KUTOENDELEZA kwa sababu unasita KUKIRI umefikia sehemu ambayo ni faida kwako ukidakwa kuliko kuendelea na usichojua, kukihitaji, wala kukifaidi.

Unaweza kufanya mpaka ukafikia kisehemu ,CHINI JUU haikupeleki MAHALI na hunapakwenda.

Cha ajabu....
....... ni KWELI kuna KA ahueni utakokapata ukishafumaniwa, kwa sababu huhitaji kufanya siri tena, na kwa kufumaniwa unapakwenda ambako ni kuishi na UKWELI kuwa umedakwa.

Tatizo ni..
... ukishafumaniwa na sio siri tena , unaweza kusahau, lakini maana yake unaanza upya na mara hii unaanza kuishi HUKU kila mtu anajua kuwa wewe mwizi halafu ni kweli unabusha ,ndio maana unapenda kuvaa kanzu.

Starehe ya kufanya kwa siri ni tamu mpaka ifikiapo wakati umezoea sana KIDOGO kufanya kwa siri mpaka imechosha au haikusisimui tena kama jana, na unataka kubadili staili ya kufanya kwa siri.

Kufumaniwa kunaweza kukawa ndio suluhisho la tatizo lako la kuendeleza kautamu ulikoanza kukakinai kutokana na kufaidi kwa staili ileile , uchochoro uleule tu, wakati labda juu ya meza nako kungefaa siku nyingine, kama jamvini kusivyofaa kulia UBWABWA tu.


Binadamu kama binadamu ni rahisi kusahau, hata kama kusahau ni kwa KUSAHAU maumivu ya kufiwa na KUKU wako Mpenzi.

Njaa ikianza kuuma tena, kumbukumbu ya chakula kizuri ulichowahi kula msibani juzi, ni kumbukumbu za mbali sana tu na zikusaidiazo kuendeleza kukutaabisha tu. .

Lakini...
.. Ni kweli kumbukumbu zako hata kama sio nzuri sana UKIBAKWA, huwezi kusahau, KUMBUKUMBU zipo na ndizo zinaweza zikawa KICHOCHEO cha mwanzo wako wakujiadhari na WANADADA kwa sababu ni liMWANADADA lilikubaka.

Kumbukumbu zako za jinsi ulivyoaibishwa , hata kama unasema unazikumbuka leo kama vilevile ilivyokuwa wakati wa tukio, inawezekana kuna mawili masita zaidi ambayo yalitokea nyuma ya kisogo chako ambayo uliyaona na huyakumbuki , ambayo yanakusababisha mpaka leo uogope MIJUSI ingawa huelewi kwanini unaogopa mijusi kama uogopavyo mende tu.

Swali:

  • Kama umefikia ukingoni na unadhani hakuna ujanja, si FUMANIWA tu YAISHE?

UZURI wa kufumaniwa ni kwamba, hauna ujanja, bali UNALAZIMIKA kuanza UPYA, kitu ambacho ni kizuri kwako kwa sababu labda usingekuwa na msukumo wa kuanza upya.

Kuishi na siri , utamu wake ni jinsi unavyoweza kujistukia ulivyokuwa na akili , hasa kwa kujaribu kuhakikisha watu hawastukii siri yako kuwa wewe MCHAWI halafu mwanamke mzima hujatahiriwa wakati nia yako utahiriwe kidoooogo!

Ukifumaniwa nishai ,watu wanaweza wakastukia kuwa wewe BOMBA la MTU na ndio ufunguo wa kwenda MBINGUNI ya kwenye MDUNDIKO.

Kuishi na siri si lazima kuwe kutamu ,hasa kusababishavyo ushindwe KUZINI hadharani kisa wewe MPAGANI au kula KITI MOTO mbele za watu ,kwa sababu wewe MUISLAMU na nguruwe ni haramu ingawa ndio nyama yako kipenzi kama NANIHII au MSABATO tu.

Lakini..
.. Ukifumaniwa unaweza kupigwa, SHAURI YAKO!

DUH!
NAacha!
Wikiendi NJEMA!

Ngoja PATRICK Saint ELOI aseme MAGNIFIK

Au tu JACOB F. DESVARIEUX aseme GOREE

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

MARKUS MPANGALA 5:46 pm  

Fikra, falsafa na mambo mengine nyomi. Kufumaniwa ili yaazne ikop kazi, lakini ukifumaniwa utaanza tena? ushanogewa utaacha? kuiba kutamu lakini utaiba hadi lini? Basi fumaniwa ili yamalizike, loooh nifumaniwe na mke wa mtu ili yaanze? mmm utakuta tunafanya mambo kwa ksingizo eti shetani tu!!! kanipitia ebo uliponogewa na kudharau ndoa yako, uliponogewa na kuona unapata kumbe umepatikana!! alah kumbe umezoea vya kunyonga, basi fumaniwa tu uchinje kabisa siyo kunyonga? eboo! kumbe unaiba mke wa mwenzio nawe ukifanyia hivyo je? bora UFUMANIWE ILI YAANZE na mwenzio atafute mwingine kuliko kujigeuza Mbeta ya Ulanzi.

Christian Bwaya 10:28 am  

Kitururu habari za siku?

Siku ya kublogu leo. Tukiiadhimisha kwa kutembelaana itatuunganisha zaidi. Long live JUMUWATA!

Simon Kitururu 6:25 am  

@Za siku si mbaya Ubze kidogo tu!
Samahani nilitingwa na shugjuli ndani ya siku. JUMUWATA inahitaji kufufuliwa na ikibidi, uongozi mpya uchaguliwe kuipa nguvu ya kuondokea spidi.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP