Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

BINADAMU ni MBAGUZI na asingekuwa MBAGUZI LABDA asingejali kuwa SURA ya KIMWANA MZURI ina pua kama JIPU!:-(

>> Thursday, August 26, 2010

Na haki ya nani tena BINADAMU huchagua ni nini  ni UBAGUZI wa kuulalamikia,...
.... ndio maana UBAGUZI wa VYUO au SHULE TU FULANI wa kuchagua waliopasi tu MTIHANI huwa hauonekani kuwa ni UBAGUZI.:-(


Haki ya nani tena LABDA hata kuchagua wafanyakazi  kwa kudeku uzoefu wao katika kazi aka EXPERIENCE ambao WANAFUNZI huulalamikia,....
.... ni ubaguzi tu  ingawa ampandishaye cheo MFAGIZI WA CHOO kuwa meneja wa CHOO CHA STENDI kisa siku hizi ni MZOEFU kuhusu maswala ya MSALANI NA HARUFU ZAKE huwa hadhani kitendo chake ni UBAGUZI.:-(


Swali:
  • Unadhani wewe sio mbaguzi tukinyambulisha ni nini KIKUTEKENYACHO kunako kwa kupenda kikutekenye ENEO ANUAI kwa hiari yako?



Ndio,...
.... labda hata uchaguzi wako wa kumpenda KISHTOBE mwenye tako jembamba kuliko  yule mwenye tako LILILOTUTUMUKA ni ubaguzi,...
.... ingawa kwa sasa  unadhani UBAGUZI ni ule tu wa RANGI, kikabila  au tu KIDINI kwa kuwa tu dini yenu ya kuamini MBUYU  inadharauliwa na waaminio dini za PESA.:-(


NI WAZO TU hili MKUU na wala huhitaji ukoko wa makande yaliyo ungwa kwa nazi ili KUPOOZA jazba!:-(

Hebu ERIC DONALDSON abadili kitu kwa kitu-Traffic JAM




Au tu Gregory Isaacs arudie-Material Man


Au tu tena GREGORY akune kwa- Not the way



Amwage-Hot Stepper




AU tu aachie tu tena na ndude -Cool down the pace

5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 9:40 pm  

Hivi leo nimekuwa nikiangalia DVD ya kishitobe wewe kishitobe wangu hata sikuangalia kama ana tako kubwa au ndogo.

Je wale wanaoacha kuwasalimu/kuwataka hali au kuwasliana na marafiku zao au wawapendao pia ni ubaguzi? ni swali tu na nimeuliza kwa sauti tu:-(

Masangu Matondo Nzuzullima 2:18 am  

Kila binadamu ni mbaguzi. Hata Wamarekani Weusi wanaojidai kuwa wameonewa sana nao wanawaona Waafrika kuwa ni wanyonge wao na kuwadharau....

Pengine hata nadharia nzima ya Charles Darwin na hasa Natural Selection; na Struggle for Existence and the Survival of the Fittest imesimikwa katika Ubaguzi.

Kwa nini CCM na si CHADEMA au CUF pengine pia ni ubaguzi.

Pengine hata uchaguzi wa yupi aende motoni na yupi aende paradiso nao ni ubaguzi.

Kama Yasinta hata mimi nawaza tu...

emu-three 12:06 pm  

Ubaguzi ni sera ya kila mtu, ila kuna kubagua na kubagua. Ubaguzi wa kijumla unaojulikana na ubaguzi nafsi, wako mimi na wewe, ndio maana wewe ukampenda mweupe na kumuoa, au kuolewa, kwanini ukafanya hivyo?

emu-three 12:06 pm  

Ubaguzi ni sera ya kila mtu, ila kuna kubagua na kubagua. Ubaguzi wa kijumla unaojulikana na ubaguzi nafsi, wako mimi na wewe, ndio maana wewe ukampenda mweupe na kumuoa, au kuolewa, kwanini ukafanya hivyo?

emu-three 12:06 pm  

Ubaguzi ni sera ya kila mtu, ila kuna kubagua na kubagua. Ubaguzi wa kijumla unaojulikana na ubaguzi nafsi, wako mimi na wewe, ndio maana wewe ukampenda mweupe na kumuoa, au kuolewa, kwanini ukafanya hivyo?

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP