Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MTAZAMO kama SILAHA uwezavyo kumsaidia MALAYA kuvumilia maumivu ya biashara ya KUJIUZA!

>> Wednesday, August 11, 2010

MTAZAMO wa mtu juu ya KITU,....
..... ni bonge la SILAHA,....

..... ndio maana hata kuruka KICHURA CHURA kukitazamwa kwa mtazamo wa kuwa KICHURACHURA NI MAZOEZI  huwa ni MAZOEZI ,....

.... wakati ukirushwa KICHURA CHURA ukiwa na mtazamo ni ADHABU  hicho hicho KICHURA hugeuka kuwa ni ADHABU.:-(




Swali:
  • SI umewahi kuona watu katika mazoezi wanapigishwa PUSHAPU  na wanaitikia wito wa KOCHA WA ZOEZI  kwa FURAHA?


MTAZAMO ni kitu cha ajabu,.....
.... kwa kuwa unaweza kukufanya URIDHIKE hata na UMASIKINI kwa kuwa kwa mtazamom wako hicho ni kitu cha kawaida  kwa kuwa jamii yenyewe yote uishinayo ni MASIKINI na  kuona ombaomba ni KAWAIDA.




MTAZAMO ni kitu cha ajabu,....
.... kwa kuwa kwa MTAZAMO wako kama wewe unajihisi ni MBAYA hata uwe MZURI VIPI unaweza usijiamini KIUZURI kitu kiwezacho kukufanya upende kusifiwa mara kwa mara ni MZURI ili tu angalau ujiamini kuwa labda wewe sio MBAYA SANA kitu ambacho kinaweza kuhasiri hata ni NANI UNAFIKIRI NI MARAFIKI WA KWELI kwako kisa wanakusifia tako kitu ambacho kinafanya udhanie wasio kusifia kalio hao sio MARAFIKI WA KWELI na kwa kidhungu aka LUGHA YA KITAALAMU YA KIBISHOO  ukawaita MA- HATER  kama tu vile kutokusifiwa sio KAWAIDA.:-(


MTAZAMO ni kitu cha ajabu,....
.... unaweza ukakufanya usistukie MUHESHIMIWA ni MALAYA ingawa afanyacho ndicho ukiiitacho UMALAYA kwa kawaida.:-(


SAMAHANI NALIKATIZA WAZO HAPA kabla ya kuongelea kwa kina  ,....
....``MTAZAMO kama SILAHA uwezavyo kumsaidia MALAYA kuvumilia maumivu ya biashara ya KUJIUZA!´´




Swali:
  • Kwani kwa MTAZAMO wako hujanielewa naongelea nini katika kudai MTAZAMO wako unaweza kuwa ndio ukuponzao kusikia maumivu wakati ungegeuza mtazamo CHUNGU ingekuwa TAMU?





Hebu LOPANGO YA BANKA wadinye ndude kubwa KATIKA KUBADILISHA HALI YA HEWA KIJIWENI kwa kitu-MPO NA KONGO




Bisso Na Bisso nao wanyokolishe kwa kitu - Le Reve Africain






AU tu hebu tu BISSO na BISSO wamalizie na ndude-Bisso na BISSO


0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP