Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KUMBUKUMBU nishai - kwa kuwa inaweza KUGEUZA uhalisia wa kitu kwa kutanua hata UJAZO wa tako jembamba KUKUMBUKWA kama TAKO LILILOTUNA!:-(

>> Monday, August 16, 2010

Kumbukumbu si lazima ni FACT aka kwa kindengereko UHALISIA wa kidude,....

.... ndio maana TUKIO hilohilo  lililoshuhudiwa na WATU KUMI ukiwauliza hao watu kumi unaweza kupata STORI kumi tofauti za jinsi KIDUDE kilivyo tanuliwa.:-(



Na kumbukumbu za KIDUDE,...
... kuna wakati huathiriwa na UTAKAVYO TU kukikumbuka kidude,  na  wakati kidude kinatanuliwa UNAWEZA kujikuta unakumbuka jinsi tu kidude KILIVYOJARIBU kutotanuliwa.:-(

Swali:
  • Hujawahi HATA kukutana na LIMPENZI LAKO LA ZILIPENDWA halafu ukastukia lina pua kama kibuyu  kitu ambacho ni tofauti na KUMBUKUMBU ZAKO ZA LIMPENZI  ambazo kabla hujakutana naye siku hizi  limpezi HILO MAWAZONI lilikuwa na kiuno kama n'ge na pua  LENYE utamu wa kwenye  macho ambao ni  MURUA?

  •  Kwani hujawahi kurudi mahali ambapo kwenye kumbukumbu zako palikuwa BOMBA na kustukia kumbe pako na palikuwa pakawaida tu  kama sehemu za siri  ulizozichoka?



Ndio,...
.... katika WAKUMBUKAO,...
.... kuna wakumbukao kwa kuwa WANAKUMBUKA   na kuna  WAKUMBUKAO  tukio VIZURI.:-(



Ndio,...
... katika WADAIO  WAO ni VIZURI wakumbukao,...
....si lazima WOTE NI KWELI  wakumbukavyo vina UHALISIA na UHALIHALISI kama VIDUDE VYENYEWE HALISIA WADAIVYO KUVIKUMBUKA  hata kama wasimuliavyo makunyanzi ya kidude KWA MTAZAMO WAK O wanapatia vizuri.:-(



Swali:
  • AU?
Kumbuka tu ,...
... kuna uwezekano  ukumbukavyo KIDUDE inategemea na ANGLE aka KONA YA sehemu uliyokuwepo wakati unakipigia chabo kidude.:-(

Kumbuka tu,...
... kumbukumbu za aliyekipiga chabo kidude kwa juu na aliye KIPIGA chabo kidude kwa chini  WAKATI HUOHUO, kunauwezekano KUMBUKUMBU ZAO  za kidude wakati wa tukio LA MTANUO  zinaweza KUTOFAUTIANA ingawa ni kile kile KILICHOKENUA kidude.:-(


NIMEACHA na ni wazo tu hili MHESHIMIWA!
Shikamoo basi kama UMENUNA!


 Hebu MOJA kwa moja kwa kuwa niko katika mudi ya BLUES  nimuachie Samuel L Jackson amwage  ndude - Stack -O -Lee katika kubadili hali ya hewa hapa KIJIWENI.:-(



Au tu John LEE Hooker amwage hii ndude -Tupelo katika kuendeleza BLUES



Au tu tulainishe kidogo NDUDE  kwakuingizia dalili za ULATINO  kwa kumuachia John Lee Hooker akija tena na SANTANA wakijamba kisanii kibuyu - The Healer





Au tu na  JACOB F. DESVARIEUX alainishe kwa kunakishi BLUES kwa ZUKU MUZIKI katika mkito-Euphrasine's Blues




NAKUTAKIA JUMATATU YENYE matako manene MHESHIMIWA hasa kama wewe ni mpenzi wa SANGARA WAMO!:-(

7 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 11:47 am  

"NAKUTAKIA JUMATATU YENYE matako manene MHESHIMIWA hasa kama wewe ni mpenzi wa SANGARA WAMO!:-(" hapa ni kaazi kwelikweli duh! nilikuwa nafikiri watakatifu ni watakatifu kweli lakini.....

Simon Kitururu 12:02 pm  

@Da Yasinta: Kwani UTAKATIFU unazuia mapenzi ya tako?

emu-three 1:52 pm  

Nimeokota kidude...ni wimbo wa kushadihisha, ingawa kidude hicho kikawa sivyo ndivyo unavyochokonoa kwenye ubongo.
Kwa mtoto wa mjini mwenye kuvaa nusu tako, anaweza kuiita ngombe zinga la mdudu, ama kachanga ka mawazo kanaweza kumkosoa na kusema sio lidude ni kidude, na kidude kwa kipare ni funza alitoholewa na mdudu!

nyahbingi worrior. 4:27 pm  

Simon.........

EDNA 7:20 pm  

Hehehee,KIDUDE,tako JEMBAMBA....haahaa you really made my day.

Simon Kitururu 8:16 am  

@Emu -Three: Wewe Mpare nini kama mimi?:-(
@Rasta LUHIAMU: Nyahbingi 2orrior.......
@WDNA: Nahisi wewe mtundu kama umechekeshwa na hii ndude.:-)

Yasinta Ngonyani 5:09 pm  

Simooonnnnn! ;.(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP