Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kama kuna LA MUHIMU katika CHEMBECHEMBE za busara zilizoko kwenye UJINGA.:-(

>> Sunday, August 15, 2010


Operesheni za MJINGA,...
.... kwenye DARUBINI usishangae kustukia hazina UJINGA.:-(

Na kwa WEREVU ukitafuta wao UJINGA,....
..... wawezakuta mpaka TANI ELFU za UJINGA.:-(


Na katika UFIKIRIAYO ni mambo ya KIJINGA,....
...... yaweza kuwa ni kweli TU KWAKO kuwa ni ya KIJINGA kwa kuwa TU umeshaamua HAYO ni ya KIJINGA.:-(

Na labda UKITAFUTA busara na UEREVU  katika  yadhaniwayo ni ya KIJINGA,....
.....waweza ibuka MWEREVU na mwenye BUSARA na wala sio MJINGA.




DUH! NASITISHA WAZO hapa  !:-(
KUMBUKA hapa na spekuleti  tu HOJA katika WAZO KIJEBA na wala usibanwe chupi kama HUNIELEWI!:-(



Hebu jikumbushe kitu katika -Think DIFFERENT


Au hebu jikumbushe pia katika -Information Overload


Au turudi tu CONGO ili LOPANGO ya BANKA warudie ndude -MPO NA KONGO

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 6:04 pm  

mmhhh:-) jumapili njema kaka Sim sim:-)

malkiory 8:21 pm  

Information overload ni shule ya kutosha!

Simon Kitururu 2:28 am  

@Yasinta: Asante Dada!
@ Mkuu Matiya: Si utani!

emu-three 2:25 pm  

Hivi ukimuona jamaa yupo kwenye maabara anachezea mavi siunaweza kuuita ujinga, kwanini mtu achezee kinyesi, lakini kwake ni taaluma yenye faida kwa maisha ya binadamu.
Wapo wanosomea kutibu wagonjwa wa akili, ambao kubwa zima linaendesha gari,mmmmh, wao utauita ukichaa, lakini anayesomea kwake humpa heshima, na kuitwa dakitari...
Ujinga kwako, kwa mwenzako inaweza kuwa werevu.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP