Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Labda USIMTISHE MTOTO wako!

>> Thursday, August 05, 2010


Kuna kitu WATU wengi hawajui kuhusu MIE Simon KITURURU,...
... ila ukweli ni kwamba mkono wangu wa kulia haufanyi kazi vizuri kama inavyotakiwa ,...
... kwa KIFUPI hata UKIWA  sio mbali sana siwezi nikakurushia jiwe  kama nataka kukubwenga JIWE kirahisi na MKONO WA KULIA.


Na tatizo lilianza kisa nilikuwa naficha siri eti kwa kumuogopa BABA.:-(

STORI fupi laini na YA KWELI :

Tulikuwa tunaishi SONGEA na moja ya vitu MDINGI alikuwa hapendi ikiwa pamoja na KUWA MCHAFU , kufeli mtihani enzi hizo nikisoma SHULE ya MSINGI MFARANYAKI (kitu ambacho nilikuwa sifeli) ,....
..... nilikatazwa kupanda juu ya MITI aka kuparamia miti kimichezo.

Siku moja mie na marafiki zangu tukaenda  kuiba maembe  aka KUTUNGUA MAEMBE yasiyo yetu shambani  kwa  WANAFUNZI WA SONGEA GIRLS. Enzi hizo shamba la songea GIRLS lilikuwa kubwa  na sisi tulikuwa tunaingilia upande wa UWANJA WA MEDICAL  karibu na nyumba za mwisho mwisho za walimu enzi hizo za miaka ya NAINTINI EITEZ( (Kumbuka ni miaka mingi sijafika Ruvuma sijui maeneo hayo yakoje siku hizi)


Basi BWANA katika kuwinda maembe bolibo na embe sindano  tukaupata mti ambao mbivu zilikuwa zimenona juu kabisa. Na mie ambaye hukatazwa kupanda miti nilikuwa kiongozi kuparamia juu kabisa kutikisa mti.

Kilichotokea ni kwamba,...
.... katika kutikisa tawi ili kudondosha maembe  tawi likakatika na kilichofuata nilijikuta chini nikijiuliza niko HAI au NIMEKUFA,.....

.....na chaajabu hata marafiki zangu wakinisemesha nilikuwa siamini kama niko hai kwa KUWASIKIA kwa kuwa nilikuwa nahisi kuwa labda hata MFU akisemeshwa huwa anasikia.:-)


Katika kufupisha stori hii ya kweli;...
 ....nilivyoanguka nilitegua mkono wa kulia na baadaye nikaja stukia labda na kitu kingine mkononi kiliharibika.:-(

KIKUBWA:
Kwa kuwa kwanza nilikatazwa kupanda miti na PILI miye na marafiki zangu tulikuwa tunaiba maembe ya wana SONGEA GIRLS nilifikiri sio busara kusimulia hicho kitu nyumbani. NILIFICHA maumivu na ugonjwa  kisa NAMUOGOPA BABA....
.....na kwa bahati nzuri ilikuwa ni kipindi cha baridi SONGEA na maswala ya SWETA na JACKETI pamoja na MAIGIZO kuwa NIKO BOMBA  yaliniwezesha kuficha nimeumia mpaka mkono ukapona kinamna.

TATIZO ni kwamba mkono ulivyopona mpaka leo hauwezi  kumlenga MBAJUWAYU  bila msaada wa mkono wa kushoto.


Kwa kifupi :
Nilijitia udhaifu wa mwili KWA KUFICHA UGONJWA kisa NAOGOPA KUCHAPWA. na BABA:-(
Unajua tena AKILI ZA KITOTO!:-(

NI moja tu ya stori ndogo ya KUJARIBU kukufanya MHESHIMIWA ufikirie kabla hujamfanya mwanao AKUOGOPE mpaka ashindwe kukutaarifu hana pesa za kutoa mimba kwa hiyo atajikorokochoa mwenyewe kisiri bafuni.:-(


Na ni HILO TU MKUU!

Hebu OCHESTRA MAKASSY wadunge ndude-MKE WANGU


Hebu NDALA KASHEBA arudishe ndude-MARASHI YA PEMBA




AU hebu tu DDC OCHESTRA Mlimani PARK wakite kwa -MTOTO AKILILIA WEMBE

Baadhi ya PICHA zaidi...

Photobucket




Photobucket




Photobucket




Photobucket



Photobucket




Photobucket




Photobucket





Photobucket




Photobucket




Photobucket





Photobucket




Photobucket



Photobucket




Photobucket



Photobucket



Photobucket




Photobucket




Photobucket





Photobucket





Photobucket




Photobucket




Photobucket



Photobucket




Photobucket




Photobucket



Photobucket




Photobucket

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

malkiory 2:08 pm  

Ni ujumbe mzito bwana Kitururu! kama mzazi ninaupokea kwa mikono miwili.

emu-three 2:31 pm  

Paamoja na ujumbe nimegundua zaidi ya hayo hata katika kuandika kwako unapenda sana kufichaficha kile unachotaka kukilenga, au hulka imeota mizizi.
Sio kwamba ni makosa, bali ni kipaji cha hali ya juu kama malenga wa vitabu vya kale

Yasinta Ngonyani 12:32 am  

ujumbe umefika na umetulia kweli. Ahsante kaka Simon..

o'Wambura Ng'wanambiti! 5:43 pm  

Dah! somo limetulia!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP