Unaweza kurahisisha KUWAUMIZA walio HAI waijalio MAITI kwa kuipiga bonge la teke MAITI!:-(
>> Saturday, August 14, 2010
Kulengwa,....
.... sio lazima moja kwa moja ULENGWE.:-(
Swali:
- Unabisha?
Ndio,...
....moja ya STAILI ya kumuumiza MAMA YA MTOTOO wala labda sio kulipiga MBATA mama la toto,...
.... kwa kuwa inawezekana MAMA LA TOTO litaumia zaidi kama utalibwenga bonge la konzi LITOTO LAKE alipendalo.:-(Swali:
- Si unakumbuka BAADHI ya maumivu uyapatayo wala haukuumizwa moja kwa moja WEYE?
- Si inasemekana kuna watu weusi waumiao Rais OBAMA akitukanwa kuhusu yamuhusuyo OBAMA na wala YASIYOWAHUSU wao walalahoi kisa wanajisikia yake yanawahusu kisa wanaamini naye MWEUSI?
Ndio ,...
... UKICHUNGUZA labda hata kilichokuumiza leo wala HAUKULENGWA wewe.
Ndio,...
..... na labda wakati linalengwa TOTO kwa bonge la KONZI , kushikwa BONGE la kibindo au TU pamoja na TOTO kufinywa lile BONGE LA MFINYO na LIBABA lake,....
Swali:
- Ushawahi kuhisi utamu kwa kushuhudia mwingine anagawiwa BONGE la utamu?
Ndio,....
..... inasemekana kuna watamanio hata MME wa mtu kisa stori tu ambazo zimewafanya wastukie utamu tayari wa lijitu ambalo sio lao na HAWAJA lionja.:-(Ndio,...
..... tamu kama CHUNGU VILE labda kisaikolojia unaweza kusikilizishwa hata bila kuonja WEYE mwenyewe MOJA KWA MOJA - kwa kushuhudia TU - au tu kusikia waonja TAMUTAMU - na kudhani unajua MAUMIVU ya ambao UNADHANI UNASHUHUDIA chungu wanaonja.:-(
Swali:
- SI unakumbuka kunauwezekano mkubwa MAITI haisikii maumivu?
NI WAZO TU HILI KIJEBA na wala USIKONDE kwa kuwa kunauwezekano HALIKUHUSU!:-(
Hebu tubadilishwe wazo hili na BIZMAN akirudisha ile ngoma ya mpwito ijulikanayo kama-MADEMU WA BONGO
Au tu tubakie BONGO ili RAY C naye atupe pambio-Touch ME
Au tu na Saida KAROLI anyuke-Ndombolo ya SOLO
0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment