UMUHIMU wa kutokuwanacho KIDUDE!
>> Friday, August 13, 2010
Kama huna jiulize;...
.... HIVI wenye NAVYO wana nini IKIWA hulka ya BINADAMU hufanya wenye navyo kusahau au hata KUTOSTUKIA umuhimu wa walicho NACHO na hapo ni kama wanakumbuka kidude WANACHO?
....HIVI hata WENYE amani maishani mwao YOTE kwani ni kweli wana AMANI kama hawajawahi kustukia ni nini kutokuwa na amani MAISHANI?
KUTOKUWA nacho KITU,...
....yaweza kuwa ndio changamoto imfanyayo MTU kustukia thamani ya KIDUDE.
Na wengi waliozaliwa na kukikuta KITU,....
..... yaweza kuwa hawapati hata motisha ya kujifunza ni nini thamani ya KIDUDE.
Swali:
- Au?
- SI inasemekana hata thamani ya pesa ni tofauti kwa aliyezaliwa na kujikuta yuko kwenye familia ya wenye pesa kitu kiwezacho kusumbua kujifunza kwake kubana matumizi?
- Unafikiri mwenye tako analithamini tako kama asiye natako alithaminivyo tako ?
Ndio,...
..... labda mpaka hata MSOSI huthaminiwa zaidi na wasio na chakula.:-(
Ndio,....
..... labda moja ya tatizo la TANZANIA ni jinsi ilivyopata uhuru kirahisi KWA POROJO ZAIDI kitu ambacho LABDA kinaathiri UTANZANIA wa WATANZANIA hata katika kufikiria ni jinsi gani maendeleo ya TANZANIA yapiganiwe kwa vitendo zaidi ya POROJO.:-(Swali:
- Unafikiri WATANZANIA kwa kutokuwa nacho KITU wanajifunza kitu kweli kama haliyenyewe miaka yote tokea uhuru ndio hii?
NI WAZO TU HILI lisilotimilifu MHESHIMIWA!
IJUMAA NJEMA na WIKIENDI NJEMA NJEMBA!
Katika kubadili hali ya hewa kijiweni labda USIANGALIE kideo hiki-Make Sure The Kiddies Are Sleeping Before .....usije kwazika.:-(
Au turudi tena Kameruni -Sally Nyolo arudie -Tam TAM
Tubakie hapa hapa Kameruni Bébé Manga arudie ngoma-Mota Benamaa
Au tu Bébé Manga arudie tu na kitu -Amio
3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Wanasema kuwa ukiwa nacho ndio utalalamika kuwa hakitoshi, lakini kama huna utaishia kutamani.
Mwenye kutamani, anaweza akatamani hata kile kisichowezekana, kwasababu hana, akizidisha au akipunguza haitamuathiri, ndio maana sisi hatujifunzi kitu kwasababu hatuna, zaidi ni kutamani kwa wenzetu kuwa na sisi kama tungelikuwa vile!
duh mtakatifu!
Kaka Simon! Kaazi kwelikweli!!
Post a Comment