Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MIPANGO ya KIGOLI januari VS MIPANGO hiyo YA KIGOLI mwishoni mwa MWEZI WA NANE!:-(

>> Monday, August 23, 2010

Mwanzoni  mwa mwaka waweza kukuta kila MTU ana mipango kemkem MIPYA,...

.....na hari MPYA.:-(

Na asiye na KIPYA,...
.... angalau utakuta ana mori na matumaini kuwa MWAKA HUU atafanya juhudi hata ya kuacha kuvaa chupi za mtumba kwa kuwa kwa vyovyote vile mwaka HUU atanunua KIFICHA NYETI kipya.:-(


Swali:
  • Lakini si inakumbukwa kuwa MIPANGO PEKEE bila mikakati ya utekelezaji na vitendo kuchukuliwa hatua, MIPANGO hufanana na ALINACHA tu?


Na tusisahau tu kuwa,....
....KIBINADAMU,...
....binadamu awezacho kuwa na uhakika nacho JANUARI cha weza kuwa kimekaa kinyume hata Februari.:-(

Ubinadamu NISHAI kwa kuwa,....
... eti kwa LIBINADAMU,...
.... uhakika hata wa MIPANGO YA SASA HIVI ya kuwa baadaye ya leo HII , ... hilo  LIMTU  litakaa  uchi hadharani inaweza isiwe NI YA  uhakika kuwa  LABDA  ni  kweli BAADAYE hiyo HILO LIMTU  LINAUHAKIKA  hiyo baadaye LITAIFIKIA  na litakaa uchi  ,... AU hata likifanikisha BAADAYE HIYO KUIFIKIA ni kweli ILE shughuli ya kuachia DUKA LA MZUNGU LIWAZI ni kweli  kunauhakika LITACHUNGULIWA MAENEO kitu ambacho ndicho lengo la HUYO MTU katika mpango mzima wa kukaa uchi ya huyo MHESHIMIWA  ambaye anatabia nzuri tu na wala hata hana CHEMBE ya tabia mbaya au hata  kama wewe ANA   kiburi.:-(

Swali:
  • Vipi mipango yako ya JANUARI inaendeleaje katika utekelezaji MWEZI huu?:-(


NIMEACHA na ni wazo tu hili MHESHIMIWA!

Hebu tu ZAP MAMA wabadili hali ya hewa kijiweni kwa ndude-Sweet Melodie



Zap Mama wadunge na kitu-Kwenda




Zap MAMA na Erykah Badu washushe-Bandy bandy



Au tu Q-Tip amalize tu kwa-Vibrant THING

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 11:39 am  

Mipango:-(
siku hizi watu wanapanga pia ni wapi watazikwa na sanduku litakuwa vipi. au pia kama atazikwa mzima au kuchumwa moto kaazi kwelikweli. mmmmmhh ngoja niache....

emu-three 2:08 pm  

Ingefaa Mipango ije baada ya utekelezaji , yaani tuikute January kwanza tutekeleza kwanza halfu mipango inafuata, kwasababau mipango mingi inaishioa hewani, kama kubeba barafu mkononi Ubungo kwa ajili ya kuilamba Morogoro!

o'Wambura Ng'wanambiti! 4:25 pm  

Mi sina mpango na chochote...lol!

malkiory 2:33 pm  

Kitururu: Mada yako ni darasa tosha, mwenye macho haambiwi tizama.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP