Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MAPENZI ni yaleyale hata kama WIMBO WA MAPENZI LEO ni mwingine!:-(

>> Thursday, August 12, 2010


MAPENZI ni YALEYALE  hata kama ni siku nyingine na MPENZI ni YULEYULE.:-(

KITU mapenzi ni kile kile kwa kuwa HAKUNA PENZI hata wakati unapenda LINASALO TAMU YA PENDO LEO  ili iwe tamu VILEVILE kesho hata kama MPENZI ni yuleyule.:-(


SWALI:
  • Unabisha?
  • Si labda MPENZI WAKO YULEYULE ASIYE NA KIBIONGO  ni juzi ndio alikuwa TAMUTAMU ZAIDI  kwa staili ileile ya kukuna NAZI katika kibinda nkoi?



Umpendaye LEO kwakuwa MTAMU SANA leo,....
... kama unakumbukumbu nzuri tu  UNAWEZA KUSTUKIA siku moja KUWA  hata PENZI HILOHILO na MPENZI HUYOHUYO ,....
......tamu ya JANA  labda haifanani na TAMU YA LEO  YAKE HUYO MPENZI  ingawa labda tamu ya KESHO KUTWA na MPENZI HUYOHUYO inaweza kuwa ina UTAMU wenye tako kubwa  zaidi kitu kitakacho kukufanya KESHO KUTWA iwe siku ya kufikiria kwako  KUMUOA au KUOLEWA NAYE  huyohuyo  ambaye mara ya kwanza ulistukia ananuka mkojo kwa mbali  INGAWA SASA YA KESHO KUTWA UNAJIAMINISHA KUWA  ni kweli MKUSANYIKO WA TAMUTAMU ZA TABIA mpaka KITUNZA UTAMU CHAKE  KIKUCHOCHEACHO USIKILIZIE UTAMU  kwa utamu wa kesho kutwa KINAFAA KWAKO kiwe ni chako  PEKE YAKO kibahiri.:-(

LOH lione vile!




Swali:
  • SI umestukia lakini kuwa HATA mpenda UKOKO kuna siku UKOKO ni MTAMU ZAIDI ingawa kuna siku chaguo lake la kuonja ni UTANDU ingawa UKOKO ndio kipenzi chake?

NIMEACHA, na ni wazo tu hili MHESHIMIWA!


Hebu EDDIE MURPHY aongee tena katika RAW 1987akiongelea-WOMEN



Au hebu tupate Conspiracy theory katika- Moon Landing HOAX




Tupate pia Conspiracy theory nyingine ya - 9 /11 hoax



Au tu Public Enemy warudie -Dont believe the HYPE



Au tu PUBLIC ENEMY wamalize mshawasha kwa -He got GAME

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

MARKUS MPANGALA 7:48 am  

Mkuu! si unakumbuka kila kionjeo kinahisi utamu wa utandu lakini kikijeruhiwa kinahisi maumivu badala ya utamu?

UNABISHA? kama jana ulijikata na wembe halafu leo ulipendalo lako penzi la mpenzi likikuchokonoa ulipojikata na wembe halafu nikakulegezea jicho la gololi na kukuna ulipojikta na ile poooooleee ya mbaliii ukahisi kuwa kitoweo cha ngadu ni ugali wa muhogo wakati ni chachandu ya kuonjea kionjeo cha hamu.

WAZO. maisha ni nini? labda kila kionekanancho kinawazika na kujiwazia ndiyo MAWAZONI ni raha kwelikweli kubandua plasta kwenye donda ndugu halafu lipendalo kukuonja kwa kutumia kionjeo cha kukuniga roba ya huba na kukugeuza nazi kukunwa pengine linajua kuwa unahisi daktari wa zahanati anafanya tiba ya kupunguza munkari wa maumivu.

lakini nini hasa kijulikanacho kuwa maisha lakini tabia zikawa zinawakilsiaha watu? tuanze hapo...........

Mkuu ni wazo tu hili na Ruksa kulibishia. Chukua tano shaaaaa za hewani, uwe na muda mwema jemedari

Maisara Wastara 10:54 am  

Hili wazo limepinda.......

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP