Kwa kuwa PROFESA MBELE sio ISSA MICHUZI!:-(
>> Saturday, August 28, 2010
Katika kijiwe nilichopitia MUDA si MREFU,...
.... moja ya hoja ilikuwa ni UFANANISHAJI na umuhimu wa wafananishwao katika JAMII.:-(
Kwenye MABLOGA wa ki -BONGO ambao wanatujumlisha na siyeMABLOGA ambao sio warefu,....
.... ikaanza hoja ya kwa nini kuna WABONGO waendao zaidi katika BLOGU fulani fulani kuliko BLOGU NYINGINE ambazo kuna wadaio ndizo zimeenda shule zaidi na kunasa BUSARA ZAIDI kuliko BLOGU ambazo wanahisi labda hazina mchango muhimu sana kwa JAMII .
Swali:
- Unafikiri ni kweli watu wote kwenye jamii, uonalo ni muhimu WEWE ni lazima na wao walione ni MUHIMU?
Moja za BLOGU maarufu na wafananishwao ikawa ni pamoja na blogu ya Lady Jay Dee, Kaluse na busara zake, Profesa Mbele , Mjengwa na Anko Issa Michuzi bila kumsahau Chemi che Mponda, Dina Marios, Dinah wa DINAHICIOUS, Matondo , Mubelwa Bandio,Muzee wa Lundu NYASA, Edo Ndaki,..,...,... Matiya William Malkiory,...na wengine wengi.:-(
Mengi yaliongelewa na kila MSHABIKI alikuwa na lake ni kwanini KALUSE ni zaidi ya BWAYA, au Yasinta Ngonyani ni zaidi ya Matondo Nzuzullima,.....
.... bila kusahau kuwa mjadala ulinoga pale WASHABIKI wa Profesa Mbele walivyo kuwa wanadai kuwa Profesa Mbele Mchango wake ni mkubwa kuliko wa Issa Michuzi kitu ambacho kilijibiwa na hoja kama:..
....kwani mchango wa Issa Michuzi kama ni mdogo kwanini hata akilini kwako kanasa MPAKA kila ukitaka kujua YA BONGO moja ya kifusi cha habari za bongo ukifukuziacho ni hichohicho cha Mkuu wa Wilaya aka Issa Michuzi....nk..Swali:
- Kwa ni haiwezekani kuwa kila mmoja mchango wake ni muhimu kwa auhitajio?
- Kwani mchango wa Mama mzazi na wa Baba mzazi lazima ufanane kwa kufananishwa kwa kipimo kimoja ki umuhimu wao?
- Hivi ni kwanini watu hupenda kushindanisha vitu NA WATU hapa duniani , na kama napenda miziki ya Profesa J kwani inamaana ni lazima Profesa J awe ni mkali kuliko Mwanafalsafa au AY ?
Hoja hizi za nani zaidi ZIMENISHINDA na mpaka leo ukiniuliza siwezi kudai najua ni nani zaidi kati ya Peter Tosh na Bob Marley, Lady Jay Dee na Ray C, Tatunane na Watafiti, SINDIMBA na MDUNDIKO, ....:-(
Swali kidogo zaidi:
- Hivi Rais Mwinyi na Rais Mkapa nani zaidi?
- Kwani unauhakika Nyerere alikuwa ni zaidi ya KAWAWA kwa Nyerere?
NI HILO TU MKUU!
Na hebu nijaribu tena kujaribu kustukia ni nani zaidi kati ya Bob Marley na Peter Tosh wakati najua hakuna watu wawili duniani wawezao kushindanishwa kwakuwa naamini hakuna watu wawili WALIO sawa.:-(
Hebu Bob Malya arudie -Crazy Baldhead
Au tu Peter Tesha akune kwa ndude-Mama Africa
8 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Mmmmh! Ama kweli kaazi ipo sikujua kabisa kama kuna kushindana katika kublog nilichodhani ni kwamba wote tuna nia moja ya kufikisha ujumbe kwa jamii. Lakini sikuwa kabisa na hili la nani ni bora kuliko nani. Ahsante Mt.Simon kwa matembezi yako na kukuta malumbano hayo na pia kwa kutokuwa mchoyo.
Mie nadhani ni ufinyu wa mawazo kujaribu kufikiri hayo. Kila bloga anablog kwa interest binafsi. Lakini kila blog naamini huwa na mchango fulani muhimu. Kupitia blogs tunapata maarifa ambayo tusingeyapata darasani.
Mtu mmoja aliwahi kuniuliza nani mkali kati ya Sidney Sheldon na Mario Puzo. Nilimjibu mkali ni yule unayemsoma wakati huo.
Mie mabloga wote nawaona wakali tu ndo maana wanablog.
Kuna wakati nilidhani kuwa maoni mengi katika blog ni dalili kuwa inasiomwa na watu wengi...... kumbe sikuwa sahihi, kuna watu wengi sana wanasoma blog tena wengi wa kutosha.
Kwa upande wa umarufu, sina uhakina na hilo, lakini nadhani kila mtu ni maarufu katika anga zake kwa maana namna anavyofikirisha watu.......
Mtakatifu, mjadala huu uko wapi? Naomba link.
Ningependa turejelee maoni makini ya Evarist Chahali aliyoyatoa katika hoja inayofananafanana na hii kule kwa Mzee wa Changamoto. Maoni hayo hayanapatikana hapa:
http://changamotoyetu.blogspot.com/2010/05/shule-shule-shule-twafunzwa-tufunzapo.html
Juzi nilitazama kipindi cha TV hapa kilichokuwa kinalinganisha eti serial killer yupi ndiye alikuwa "mkali" zaidi ya wengine. Binadamu!
nasubiri wenye imani wamalize kwanza kubishana SWAUMU ni haki au siyo haki na ina uhusiano gani na mungu.
@Masangu Matondo Nzuzullima: Mjadala haukuwa mtandaoni.:-(
@Wote: Mmmmmhhh!
Mt. Simon kama hakuwa mtandaoni ulikuwa wapi? Je huwezi kutupeleka huko ilinasi tuungane nao?....Kapulya kwani nilikuwa nami nijue ni link gani hiy????
Kitururu: Pamoja na kuchelewa kuweka kalamu, nadhani gossiping nayo ni sehemu nzuri tu ya kujipatia feedback. Nadhani michango ya wadau itakuwa ni chachu katika kumaliza ubishi wa mdahalo uliozuka kijiweni.Cheers!
Post a Comment