Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Katika kujaribu kutojisahaulisha kuwa KUNA WENGINE hapa duniani wenye MENGINE!

>> Wednesday, November 17, 2010

Na katika KUJISAHAU,.....
....unaweza KUSAHAU kuwa kuna  WENGINE  hapa DUNIANI ambao sio WEWE na labda kwa kuwa hao sio WEWE,...

........hawaoni na KUFANYA mambo kama wewe.:-(


Swali:

  • Lakini si inasemekana labda mpaka AMANI MOYONI mwa mtu huchangiwa pia na MTU anajikubalije yeye mwenyewe halafu pia ANAKUBALIJE watu wengine ambao hawaoni wala kufanya mambo kama YEYE?

  • Na si inakumbukwa kuwa,....
....SIRI ya AMANI kwa wengi ni kujaribu kuelewa wengine ambao kimitazamo hata ya ni nini babu kubwa msalani katika swala la  KUCHAMBA  ni tofauti?

Na labda tu ili kutojisahau,....
... ni vizuri tu kukumbuka MTU mwingine hata kama ni nduguyo,....
..... bado ukweli uko palepale kuwa huyo si WEWE,...
..... kwa hiyo jaribu kumuelewa tu  kivyake kwanini hata katika mambo madogo madogo kama ya kupenda ugali wa mihogo kwa MLENDA  hamuonani jicho kwa jicho KIKIKUNOGEWA.:-(

Ni wazo tu hili BINGWA!

H
ebu Kasse Mady Diabate atukumbushe The art of AFRICAN story telling katika - Kela Djeliya  HAPA

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP