Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kihalihalisi NYOKO iwezayo kuwepo ndani ya kujaribu kufananisha NYUMBA ya GAVANA wa BENKI ya TANZANIA na nyumba za akina SISI hohehahe!:-(

>> Friday, November 12, 2010Kuna uwezekano,...
....TAKA -usitake,...

.... Nyumba ya mfanyakazi wa nyumbani wa RAIS wa TANZANIA,...
..... na ile ya mfanyakazi wa nyumbani wa MWALIMU wa SHULE ya msingi ya MATOMBO  MJINI,...
...huko Morogoro,...
.... haziwezi kufanana kirahisi.:-(

Swali:

  • AU?

Ndio ,...
.... wote twajua kuwa UWEZEKANO upo pia wa NYUMBA ya ombaomba MAARUFU TANZANIA ,...


....Mheshimiwa MZEE Anthon MATONYA......
Mzee Anthon Matonya kama nilivyoikuta Dullonetwork
 ......kiuthamani inaweza kulingana tu na ya Rais KIKWETE kama Rais KIKWETE akiamua kuwa na nyumba yenye thamani kama ya Mzee MATONYA,....

.... hasa kama  kimaadili yeye MTUKUFU RAIS hathamini sana  nyumba za ghali,....
..... ila UKWELI utabaki pale pale kuwa ,... 
.... kihali halisi kama kipimo ni kiasi cha fweza ziwezazo tumika katika kununulia aina ghali ya vyoo visaidiavyo kitendo kilekile cha kwenda haja kubwa,...
....NYUMBA ya KIKWETE haiwezi kirahisi ikawa sawa na ya Mzee MATONYA.:-(Na unaweza ukaniuliza ni kwanini naandika hivi;....

....Hivi karibuni nimekutana sana na BLOGU  ambazo zinafananisha NYUMBA ya GAVANA wa BENKI ya TANZANIA na nyumba za WALALA HOI wengine  TANZANIA.

Kama uonavyo hata hapa kwa NANGONYANI.Cha kujiuliza tu:
  • Hivi ni KWELI KIHALIHALISI  inaweza aminika GAVANA wa BENKI kuu atakuwa na NYUMBA inayofanana na MAMA NTILIE wa KIBAHA  uchochoroni kweli?
  • Hivi si kuna uwezekano KIOMBAOMBA Tanzania kunawatakaodai HATA Mheshimiwa Anthon MATONYA ligi yake ni kubwa kitu ambacho labda kihalihalisi OMBAOMBA wengine ni COROLLA ya mtumba kama Mzee MATONYA ni BENZI mpya ya kifisadi iliyoruka USHURU Tanzania?
  • Hivi ni kweli wakati mwingine tunavyolalamika , haiwezekani kuwa tuyalalamikiayo PAMOJA na ukweli wake labda ni  kinyume na   silika ya KIBINADAMU hasa tuongeleapo usawa wa BINADAMU hata kama ni katika kuwalinganisha YESU na Mohammed?

Ndio,....
..... katika NCHI MASIKINI kama TANZANIA ambayo hata kulipa mishahara ya wafanyakazi wa SERIKALI inategemea MISAADA ya WAFADHILI,...
.....ni UJINGA kutumia fedha KIUFUJAJI katika mambo yasiyo muhimu  .:-(


Ndio,...
..... najua yasemekana TANZANIA na WATANZANIA kwa ujumla,...
.... tuna matatizo ya kuchagua vya kukipa KIPAUMBELE,...
..... kitu kiwezacho kufanya MTUZ KIBAO zikaupa UGALI WA SEMBE  kipaumbele kuliko UGALI WA  DONA la unga usiokobolewa wenye nguvu kama MFUNGWA aliyekuwa jela muda mrefu  aliyetoka tu jela na   kupata tu DEMU HALLAL aka MKE  kiunyumba ,...
....kijuhudi au KIMUNKARI kama kipimo cha nguvu katika kufanikisha SHUGHULI.:-(

Lakini;
  • Je, wakati tunalalamika huwa tunaingizia katika MNYAMBULISHO  hali halisi ya jambo katika  kudhania kuwa kwa kuwa TANZANIA NI MASIKINI kwa hiyo basi na KIONGOZI MTUKUFU  Waziri MKUU PINDA  matatizo  ya baiskeli yake ya SWALA yawe sawa tu  na ya Mwenyekiti wa Nyumba kumi kumi wa mtaa wa akina KABORIBO kule UPARENI aka  kijijini MBAGA ,  SAME ?

Hebu tudeku nyumba ya gavana kama  nilivyo ikuta HUKU kwa Da YASINTA....Na darasani kwa Maprofesa wa baadaye kutoka huko huko kwa Da Yasinta ....


NAENDELEA KUWAZA.......!:-(

Ijumaa na WIKIENDI NJEMA Mheshimiwa!Hebu tujikumbushe AHADI zilivyo RAHISI katika  KUAHIDI TU kwa kudeku tena ufundi wa Rais OBAMA katika kuahidi...


Au tudeku JAMAAZ  katika kujaribu KUWA WATU WAZURI au tu katika  kujisikia TU ni watu wazuri katika sindimba-We are the WORLD

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 3:59 pm  

Kuna wakati unaweza kujisikia vibaya ukilinganisha nyumba, chakula, na hata mavazi uvaayo wewe na ukimwangalia jirani yako. Ila wanasema si vizuri kulinganisha hivyo, sijui kama ni kweli? na sijui kama ni uungwana mmoja aishai kwenye nyumba inayovuja na mwingine analala usingizi mtamu akiwa amelala kwenye godoro la bei? Upi ni uungwana hapa? mmmmhh ngoje niaache maana mihasira inakuja...vuuuumu nimetoka:-(

Anonymous 4:51 pm  

siku zote vidle havifanani,katika viganja vyetu.huwezi kulinganisha kitu alicho nacho mtufulani eti nakusema ni ufujaji wa pesa.si kweli kila mtu ana thamani yake katika ulimwengu hu wa anasa. hivyo basi nyumba ya bei mbaya aliyo jengewa jamaa,anastahili,acha kufananisha na nyumba ya mlala hoi shule kukosa madawati.subiri utakapo kuwa kwenye nafasi hiyo ndyo unaweza kujuwa kwanini iko hivyo,swali wewe umejenga,kama ndiyo thamani ya nyumba yako inatosha kununulia au kujenga shule (madawati) mawazo yetu ,kazikwelikweli.mimi kaka s

emu-three 2:29 pm  

Mhhh mkuu, nipo kwenye cafe kuifungua blog imechukua robo saa...mmmh, ujumbe umefika, nitaipitia tena!

SIMON KITURURU 10:16 am  

2Wote: Mmmh!

Pammoja sana tu!


@Kaka S espeshali:

Asante kwa kunitembelea hapa kijiweni kwa kuwa haki ya nani tena nilikuwa nadhani weye ni miongoni mwa NDUGU zangu wanikwepao kijiweni.:-(

halafu sijui kwanini nilikuwa nafikiri hivyo!:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP